Kamati ya Fedha na Uongozi ya Halmashauri ya Jiji la Tanga, leo imefanya ziara ya kutembelea baadhi ya miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri yao kwa fedha za makusanyo ya ndani. ziara hiyo ilikuwa na lengo la kukagua miradi ikiwa ni moja ya shughuli ya Kamati hiyo.
Mradi wa ujenzi wa shule ya msingi ya Bombo, mradi huu unafnyika baada ya shule hii imejengwa upya baada ya jengo la awali kusitishwa kutumika kutokana na uchakavu.
Jengo hilo la zamani lilijengwa mnamo mwaka 1902 na kuanza kutumika kama shule ya Awali mwaka 1945, na baadae kuwa shule ya Msingi. Jengo hilo lilikuwa la ghorofa moja, ndani yake lilikuwa na huduma zote muhimu za shule.
Mradi mwingine ulitembelewa na Kamati hiyo ni Duka la Dawa la Jamii, lengo kuu la Maduka haya ya dawa ni kuimarisha huduma bora za afya kwa jamii na kuwezesha upatikanaji wa dawa, vitendanishi na vifaa tiba karibu zaidi na Wananchi, kwa muda wote, ubora unaokubalika na kwa bei nafuu.
Akiiambia kamati, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Tanga, Dk Jairy Khanga alisema faida ya zitakazopatikana baada ya mradi huu kukamilika ni pamoja na Kurahisisha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwa wananchi kwa bei nafuu, kusogeza huduma ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwa wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), kuongeza mapato ya ndani ya Halmashauri na kuviondolea au kupunguza kabisa Vituo vya Umma kununua dawa, vitendanishi na vifaa tiba kwa washitiri (Prime vendors).
Mradi huu upo kwenye kata ya Ngamiani Kaskazini, barabara ya nne, unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.