Tangu 2010-2016 Halmashauri ya Jiji imetoa jumla ya hati miliki 2,897, na viwanja vipya 3,037 vimepimwa kwenye maeneo ya (Mwang’ombe viwanja 279, Usagara kijijini viwanja 128 na Pongwe 1,765, na Machui 865).
Aidha, maeneo ya Mwamboni, Masiwani Shamba, Jaje, Mwakizaro, Mwanzange na Mwakidila yamefanyiwa maboresho.
Kati ya migogoro 68 ya ardhi iliyopokelewa 58 imetatuliwa na iliyobaki 10 iko kwenye hatua mbali mbali za utatuzi. Pia kuna migogoro mingine iliundiwa tume na mkoa na mapendekezo mbalimbali ya tume hiyo yameanza kushughulikiwa.
Mpango Kabambe wa Halmashauri ya Jiji
Halmashauri imeanda Mpango Kabambe (Master Plan) wa miaka 20 (kutoka 2015 – 2035). Mpango huo umejielekeza katika kuhakikisha kuwa eneo lote la Halmashauri ya Jiji la Tanga linakuwa/linapanuka kwa kuzingatia maendeleo ya ardhi umeandaliwa ili kuhakikisha kuwa ardhi inatumika vizuri ili kuondoa muingiliano usio wa lazima kwa matumizi mbalimbali ya ardhi.
Mpango uliwasilishwa kwanza Sekretarieti ya Mkoa na baadae uliwasilishwa Wizarani kwa hatua zaidi kama sheria namba 8 ya Mipango Miji ya mwaka 2007 inavyoelekeza kupitishwa sehemu hizo kabla haujaanza kutumika.
Mafanikio;
Halmashauri imeongeza uwezo wa kuandaa hatimiliki kwa waombaji/wamiliki wa viwanda
Uwezo wa ukusanyaji wa mapato umekuwa ukiongezeka siku hadi siku
Halmashauri imeboresha mfumo wa kuingiza kumbukumbu za wamiliki wa viwanja pamoja na uhifadhi wa ramani katika mfumo wa kielektroniki
Halmashauri imeweza kutenga maeneo kwa ajili ya uwekezaji
Changamoto:
Upungufu wa wataalamu wa upimaji
Uhaba wa vitendea kazi kama magari
Wananchi kutofahamu sheria za ardhi na hivyo kuzua migogoro isiyo na tija.
Hifadhi ya Misitu na Upandaji Miti
Eneo lote la hifadhi ni Hekta 5,540, kati ya hizo Hekta 3800 ni eneo lenye maoteo ya mikoko. Aidha, jumla ya miti 8,030,000 imepandwa katika kipindi cha miaka minne kufanya wastani wa 100.4%. wa utekelezaji .
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.