Uwekezaji katika maeneo ya viwanda(industrial parks) vya kuzalisha bidhaa mbalimbali katika maeneo ya Gofu chini, Pongwe, Amboni, Pingoni (Maweni) na Neema katika Barabara ya Pangani. Kuna jumla ya viwanja 282 vyenye ukubwa wa wastani wa ekari kati 1.5 hadi 6.5 kwa kila kiwanja maeneo hayo ni kama ifuatavyo:-
Eneo la Viwanda la Kange
Eneo hili lina ukubwa wa Hekta 34.5 ambapo jumla ya viwanja 55 vinamilikiwa na Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC)
Viwanja hivi vipo umbali wa kilomita saba (7) kutoka Tanga Mjini katika barabara ya Tanga -Segera ambapo limemilikishwa kisheria kwa Shirika la Maendeleo la NDC lakini halijaendeleza. Vilevile viwanja hivi vinafaa kwa ujenzi wa viwanda kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa za nje na viwanda vinavyopendekezwa katika uzalishaji huu ni pamoja na usindikaji wa samaki, vyakula, matunda,viwanda vya mafuta,nguo,chuma,samani pamoja na vifaa vya umeme.
Eneo la Viwanda EPZA
Eneo hili lina ukubwa wa Hekta 1300 ambalo lipo eneo la Neema barabara ya Tanga Pangani, na eneo hili limepimwa ila bado halijaendelezwa.Eneo hili linafaa kwa ujenzi wa viwanda kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa za aina mbalimbali kwa ajili ya kukidhi soko la ndani na nje ya nchi. Miongoni mwa viwanda vinavyopendekezwa ni pamoja na usindikaji wa samaki, vyakula, matunda na viwanda vya mafuta,nguo,chuma,samani pamoja na vifaa vya umeme.
Eneo la Viwanda Gofu chini
Eneo hili limepimwa na lina ukubwa wa mita za mraba 7,242. Lipo maeneo ya viwanda Gofu kiwanja Na.184, linamilikiwa na Halmashauri ya Jiji.Eneo hili lina miundombinu yote ikiwemo umeme, maji na mtandao wa barabara za lami.
Eneo hili linapendekezwa kujengwa kiwanda kwa ajili ya usindikaji wa muhogo ambao unapatikana kwa kiasi kikubwa Jijini Tanga pamoja na Wilaya za jirani za Mkinga na Pangani.
Eneo la Viwanda Pongwe
Eneo hili lipo umbali wa km 15 kutoka katikati ya Mji na linamilikiwa na Kampuni ya Tanga Economic Corridor kampuni inayomilikiwa kwa ubia kati ya Halmashauri ya Jiji la Tanga na Kampuni ya Good PM toka Korea. Eneo lina jumla ya viwanja 68 kwa ajili ya ujenzi wa viwanda. Eneo hili limepimwa lakini bado halijaendelezwa kwa kuwa bado halijapata muwekezaji
Eneo hili linafaa kwa ujenzi wa viwanda kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa za aina mbalimbali kwa ajili ya kukidhi soko la ndani na nje ya nchi kama vile vifaa vya kilimo, samani,vifaa vya umeme, mbolea,usindikaji wa vyakula,viwanda vya chuma n.k.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.