Kwa upande wa huduma kwenye sekta ya elimu, tuna Elimu ya Awali, Elimu ya Msingi na Elimu ya Sekondari.
ELIMU YA MSINGI
Tuna Shule za Msingi 100 (Serikali 79 na Binafsi 21) zikiwa na jumla ya wanafunzi 57,737 (Serikali 50,163 na Binafsi 7,574). Katika shule hizo madarasa ya Awali kwa Serikali ni 79 na shule za Binafsi 21 zenye jumla ya wanafunzi 8,395 (Serikali ni 6,630 na Binafsi 1,765).
Ufaulu wa Mtihani wa Darasa la VII (2016/2017)
Ufaulu wa wanafunzi wa shule za msingi ni mzuri na umepanda kwa kipindi cha miaka mitatu kutoka 78.6% mwaka 2015 hadi kufikia 80% mwaka 2017 na hivyo kufikia lengo la BRN la ufaulu la 80% kitaifa.
Hali ya Miundombinu na Samani katika shule za Msingi
Zipo juhudi kubwa zinazofanywa na Hamashauri ya Jiji la Tanga katika kupunguza au kuondoa kabisa upungufu wa miundombinu katika shule za Msingi hususani katika suala zima la vyoo na madarasa kutokana na changamoto kubwa ya kuongezeka kwa wanafunzi wanaoandikishwa kutokana na Elimu bila malipo, katika hili Halmashauri imekuwa ikitenga fedha katika bajeti ya kila mwaka kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ikiwemo madarasa, nyumba za walimu,vyoo na madawati. Pia imeweza kujenga upya baadhi ya shule zilizochakaa kama shule ya Msingi ya Bombo na kuendelea na mikakati ya kukarabati shule nyingine.
Hali ya miundombinu na samani katika shule za msingi
Na |
Miundombinu
|
Mahitaji |
Vilivyopo |
Upungufu |
1
|
Madarasa
|
1250 |
655 |
595 |
2
|
ofisi
|
135 |
57 |
78 |
3
|
Nyumba za walimu
|
1249 |
90 |
1159 |
4
|
Vyoo vya Wanafunzi
|
2374 |
753 |
1621 |
5.
|
Madawati
|
17675 |
18569 |
0 |
ELIMU YA SEKONDARI
Katika Jiji la Tanga kuna jumla ya shule za Sekondari 43 (Shule za Serikali 26 na 17 za binafsi pamoja na mashirika ya Dini) zenye jumla wanafunzi 21,746 (Serikali ni 17,159 na binafsi 4,587) Zipo shule za 04 za bweni za seirkali na shule 11 za binafsi zenye huduma ya bweni na hosteli
Hali ya Miundombinu na Watumishi Elimu Sekondari
|
Elimu ya Sekondari |
||
Mahitaji |
Zilizopo |
Pungufu(-) / Ziada (+) |
|
Waalimu
|
829 |
1051 |
+222 |
Vyumba vya Madarasa
|
462 |
430 |
-32 |
Madawati
|
17334 |
17838 |
+504 |
Nyumba za Walimu
|
1051 |
88 |
-963 |
Matundu ya Vyoo
|
783 |
410 |
-373 |
Maktaba
|
26 |
6 |
-20 |
Maabara
|
78 |
40 |
-38 |
Mabwalo ya chakula
|
26 |
7 |
-19 |
Stoo
|
51 |
29 |
-22 |
Majengo ya Utawala
|
26 |
20 |
-6 |
Chanzo: TSS-2017
NB:
Pamoja na Halmashauri yetu kuwa na ziada ya walimu 222 kama inavyoonekana katika jedwali hapo ambao ni wa masomo ya sanaa, Halmashauri bado inakabiliwa na uhaba wa walimu wa Sayansi, Hisabati na Ufundi 101
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.