1: UJENZI WA SHULE YA MSINGI BOMBO
Shuleya Msingi Bombo ni miongoni mwa Shule tatu za Umma zilizopo ndani ya kata yaCentral. Shule ina jumla ya wanafunzi 1,036 wavulana 564 wasichana 472. Kunawalimu 18 wanaume 2 wanawake 16. Shule hii imejengwa upya baada ya jengo laawali kusitishwa kutumika kutokana na uchakavu.
Jengohilo la zamani lilijengwa mnamo mwaka 1902 na kuanza kutumika kama shule ya Awali mwaka 1945, na baadae kuwa shule ya Msingi. Jengo hilolilikuwa la ghorofa moja, ndani yake lilikuwa na huduma zote muhimu za shule.
Wanafunziwote walihama kwa muda na kushirikiana vyumba vya madarasa katika Majengo yaShule ya Msingi Mkwakwani baada ya jengo hilo kutofaa kutumika tena na hivyokusababisha msongamano mkubwa katika Shule ya Msingi Mkwakwani.
Halmashauriilianza ujenzi wa majengo mbadala mwezi Septemba 2016, kwa kujenga vyumba sita(6) vya madarasa kwa mapato yake ya ndani. Na vilevile ujenzi unaendeleawa vyumba vitano (5) vya madarasa, jengo la utawala na vyoo kwa fedha zaSerikali kuu kupitia mpango wa Lipa Kulingana na Matokeo (Paymentfor Results – P4R).
Faidazitakazopatikana kutokana na mradi huu ni:-
Kuboreshamazingira ya kujifunzia na kufundishia.
Kupunguzamsongamano katika jengo la shule ya msingi Mkwakwani
Thamani ya mradi ni Tsh. 408,707,710.00
2: DUKA LA DAWA LA JAMII
Lengokuu la Maduka haya ya dawa ni kuimarisha huduma bora za afya kwa jamii nakuwezesha upatikanaji wa dawa, vitendanishi na vifaa tiba karibu zaidi naWananchi, kwa muda wote, ubora unaokubalika na kwa bei nafuu.
Hudumazinazotolewa ni upatikanaji wa dawa zote zilizopo katika orodha ya dawaza Bohari Kuu ya Dawa (MSD) na zisizo katika orodha (Generic and BrandsMedicines), huduma ya dawa kwa wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima yaAfya (NHIF), dawa kwa jamii, Dawa kwa Taasisi za serikali na binafsi kwawaliosajiliwa kwa mujibu wa sheria.
Faidaza mradi huu ni kama ifuatavyo:-
Kurahisishaupatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwa wananchi kwa bei nafuu, kupunguzaurasimu wa ununuzi wa dawa, vitendanishi na vifaa tiba katika ngazi ya Vituovya kutolea Huduma za Afya na Kuwezesha upatikanaji wa dawa, vitendanishi navifa tiba katika Vituo vya kutolea Huduma za Afya kwa 100%.
Kusogezahuduma ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwa wanachama wa Mfuko wa Taifa waBima ya Afya (NHIF).Vilevile ni Kivutio kikuu kwa Wananchi kujiunga na Mfuko waAfya ya Jamii/TIKA kutokana na kuwa na uhakika wa uwepo wa dawa, vitendanishina vifaa tiba vituoni.
Kuongezamapato ya ndani ya Halmashauri
Kuviondoa/kupunguzakabisa Vituo vya Umma kununua dawa, vitendanishi na vifaa tiba kwa washitiri(Prime vendors).
Thamani ya mradi ni Tsh.451,000,000.00
3: MRADI WA TANGA TELEVISHENI
Faidaza Mradi huu ni kama ifuatavyo:-
Kuifahamishajamii ya wakazi wa Tanga juu ya matukio ya kiserikali na kijamii yanayotokeandani na nje ya Wilaya na Mkoa wetu Kitaifa na Kimataifa.
Kutoaelimu juu ya mambo mbalimbali, mfano Afya ya Jamii, ujasiliamali, n.k
Kuonyeshashughuli mbalimbali zinazofanywa na Halmashauri, na Baraza la madiwani (ikiwemovikao vya Baraza la madiwani)
Kuinuavipaji vya wasanii wa Tanga kwa kuzitangaza kazi zao.
Kutoafursa kwa watazamaji kuwasiliana na watendaji wa sekta mbalimbali moja kwa mojakupitia vipindi vya mahojiano (live programme)
Kutoaburudani kupitia muziki, filamu na michezo mbalimbali inayoonyeshwa na kituo.
KupitiaKituo hiki, wakazi wa Tanga na Taifa kwa ujumla watapata elimu na habari juu yafursa za ajira katika uwekezaji mkubwa unaokuja Tanga, uelewa wa kutosha juu yaTanzania ya Viwanda, na umuhimu wa kutunza na kuimarisha afya zao.
TaTVinamatarajio ya kupanua huduma zake ionekane kitaifa.
Thamani ya mradi ni Tsh.136,986,799.00
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.