Eneo lote la hifadhi ni Hekta 6,240, kati ya hizo Hekta 3800 ni eneo lenye maoteo ya mikoko. Aidha, jumla ya miti 2,300,000 imepandwa katika kipindi cha miaka miwili kufanya wastani wa 92% ya utekelezaji. Katika kusimamia suala la uhifadhi wa mazingira, Halamshauri imeanzisha shamba la miti la Mleni ambalo lina ukubwa wa ekari 161, kati ya hizo Ekari 41.5 zimeendelezwa kwa kupanda miti ya Tiki ambapo kwa sasa kuna miti ya Tiki 40,000 yenye wastani wa thamaniya Tshs 1,062,600,000.
Lengo la mradi huu ni kutunza mazingira kwa kuongeza hifadhi ya Kaboni (Carbon stock), kutumika kama shamba darasa linalohamasisha watu kupata miti yenye thamni na Kitega uchumi cha Halmashauri ya Jiji.
Mikakati iliyopo baadae ni kuendelea kuongeza eneo zaidi ka kupanda miti na kupanda miti zaidi ya mikoko katika maeneo ya pembezoni mwa bahari ili kuzuia mmomonyoko na kuhifadhi viumbe bahari.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.