• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Staff Mail |
    • Malalamiko |
Tanga City Council
Tanga City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Tanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Ujenzi
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Usafi wa Mazingira
      • Mipangomiji na Maliasili
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jiamii na Vijana
      • Maji
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Manunuzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
    • Kata
    • Mitaa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Sekta ya Utalii
    • Sekta ya Madini
    • Sekta ya Elimu
    • Sekta ya Viwanda
    • Maeneo ya Nyumba na Makazi
    • Sekta ya Misitu na Mashamba ya Miti
    • Sekta ya Uvuvi
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Usafi na Mazingira
    • Maji
    • Ardhi na Maliasili
    • Ujenzi na Miundombinu
    • Uwezeshaji Wananchi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi, Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango Miji na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Siku za Kumuona Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi Iliyoidhinishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Kanuni
    • Fomu Mbalimbali
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Majarida
    • Taarifa za Miradi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
  • TangaTV

Huduma ya Usafi na Mazingira

USAFI NA MAZINGIRA

  • Halmashauri  imejizatiti vyema katika suala la usafi ikiwa ni pamoja na utoaji wa huduma za taka ngumu kwa wakazi wake ikilinganishwa na upanukaji wa mji na makazi ya watu unaoendana na ongezeko la kuzaliwa kwa taka ngumu mjini. Kwa kutimiza azma hiyo Halmashauri inafanya yafuatayo:
  • Uboreshaji wa huduma za usafi wa mazingira
  • Halmashauri inaboresha huduma zake za usafishaji wa mazingira ya Jiji ikiwa ni pamoja na kuongeza uwezo wake katika utoaji huduma za ukusanyaji taka na usafirishaji wake. Jumla ya tani 240 huzalishwa kila siku kwa kata zote 27, Kiasi cha taka kinachozalishwa na kupelekwa dampo kimeongezeka kutoka asilimia 60 hadi asilimia 95 ya tani 140 za taka zinazozalishwa katika kata 17 za maeneo ya mjini  ikilinganishwa na kipindi cha nyuma kilichopita.
  • Usafishaji wa barabara
  • Aidha, hudama za usafishaji wa barabara kuu na mifereji mikubwa ya maji ya mvua inaendelea kufanyika mara kwa mara na kuepusha mafuriko na madhara mengine ya kiafya na mazingira kwa jamii.
  •  
  • Uboreshaji wa dampo la Mwang’ombe
  • Halmashauri imeboresha dampo la Mwang’ombe kwa kulikarabati ili kuboresha udhibiti wa taka ngumu (Controlled tipping) kuendana na mpango mkakati wake wa udhibiti taka na usafishaji wa jiji (City SWM strategic plan).
  • Upatikaji wa vifaa vya usafi

Halmashauri imepata vifaa vipya vya udhibiti taka kupitia mradi wa Tanzania Strategic City Program (TSCP) ambavyo kupitia mpango maalumu wa matumizi yake, vimewezesha Halmashauri kuanza kutoa huduma ya udhibiti taka na usafishaji wa mazingira ya jiji kwa uhakika zaidi. Hali hii imeboresha zaidi imani yao kwa serikali na pia kuongeza ushiriki wao katika shughuli za usafi kujenga kati yao mahusiano mema zaidi.

Vifaa mbalimbali vya usafi kupitia mradi wa TSCP unaofadhiliwa na Benki ya Dunia vikiwemo Wheel loader 1, Bulldozer 1, Hydraulic Excavator with rubber tyres 1, landfill Compactor 1, Tractor 3, Teller 4, Tipper Truck 1, Skip Loader 3, Skip Buckets 29, Washing machine 1, Axle weighbridge 1, Workshop tool set 1 na Environment Monitoring equipment set 1.

 

  • Kampeni ya usafi 
  • Zoezi la kampeni ya usafi (msaragambo) linafanyika katika kila Jumamosi ya mwisho ya mwezi na pia Mitaa imekuwa na zoezi la ukaguzi na ufuatiliaji wa wakazi wake. Pamoja na zoezi hili kuwezesha usafi wa baadhi ya maeneo teule kwa zoezi hilo, lakini pia linahusika na kuongeza ufahamu wa jamii, kubadili mitizamo yao na kupenda kufanya usafi ili kudhibiti magonjwa na kuboresha afya zao.
  • Elimu kwa Jamii
  • Programu ya uelimishaji jamii zinaendelea kufanyika kupitia fursa mbalimbali ikiwa pia ni pamoja na kupitia program za vyombo vya habari (Tanga TV na Redio za jijini), mikutano ya jamii, matangazo ya magari na kupitia siku ya zoezi la kampeni ya usafi wa mazingira ya kila mwezi (Msaragambo).
  • Uboreshaji wa maeneo ya wazi
  • Jumla ya maeneo 14 ya wazi (Garden and Parks) yameboreshwa na kuchangia ongezeko la miundombinu ya kijani ya jiji na pia upendezeshaji mandhari ya jiji letu.
  • Tafiti za udhibiti wa athari za Mazingira (EIA)
  • Miradi mipya yote ya viwanda, mafuta, ujenzi n.k. inaendelea kusimamiwa na kuhakikisha inafanyiwa tafiti za udhibiti wa athari za mazingira (Environmental Impact Assessment - EIA) ili kuepusha miradi hiyo kuja kuwa na madhara kwa mazingira ya jiji na afya ya jamii yetu.
  • Zoezi la msaragambo limeendelea kufanyika. Uboreshaji wa utekelezaji wa zoezi la msangambo kwa kushirikisha zaidi kata na mitaa pia ushiriki wa wananchi katika usafi na mazingira yanayowazunguka na pia katika maeneo ya jamii na maalumu.

    Kuimarisha Vikundi vya jamii 9 ili viweze  kutoa huduma za uzoaji taka na usafi na Mazingira katika kata 4 za Mabawa, Usagara, Makorora na Duga.

    Kuwashirikisha Maafisa watendaji wa Kata, Mitaa na Maafisa Afya katika kuhakikisha maeneo yao yanakuwa safi

    Hatua nyingine zinazochukuliwa katika kuboresha usafi wa mazingira:

    Aidha kazi ya usafishaji wa mifereji ya maji ya mvua imefanyika kwa mifereji iliyopo kando ya barabara za katikati ya jiji

    Barabara: Barabara za Taifa, Karume, Ngwilizi, Pangani, Jamhuri na Korogwe

    Maeneo ya Makazi na Biashara:Katika kata za Central, Ngamiani Kaskazini, Ngamiani Kusini, Makorora, Majengo, Msambweni, Nguvumali, Usagara, Ngamiani, Mabawa, Chumbageni, Maweni na Tangasisi.

    Masoko: Masoko yaliyohudumiwa ni Mgandini, Makorora, Ngamiani, Mlango wa Chuma, Majani mapana na Gulio la Tangamano.

    Maeneo muhimu yanayozolewa taka ni: 

    Masoko: Masoko yaliyohudumiwa ni Mgandini, Makorora, Ngamiani, Mlango wa Chuma, Majani mapana na Gulio la Tangamano.

    Maeneo ya Makazi na Biashara:Katika kata za Central, Ngamiani Kaskazini, Ngamiani Kusini, Makorora, Majengo, Msambweni, Nguvumali, Usagara, Ngamiani, Mabawa, Chumbageni, Maweni na Tangasisi.

    Barabara: Barabara za Taifa, Karume, Ngwilizi, Pangani, Jamhuri na Korogwe

    Aidha kazi ya usafishaji wa mifereji ya maji ya mvua imefanyika kwa mifereji iliyopo kando ya barabara za katikati ya jiji

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ. March 09, 2025
  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA JIJI TANGA September 27, 2024
  • TAARIFA YA MSIBA September 18, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 26, 2024
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • TANGA: MABORESHO DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KUANZA FEB. 13, 2025

    February 04, 2025
  • MENEJIMENTI WAPONGEZWA UTEKELEZAJI MIRADI, UMALIZIAJI WA VIPORO.

    February 04, 2025
  • AFUA ZA LISHE ZAFANYA VIZURI TANGA JIJI

    January 24, 2025
  • KAMATI YA FEDHA NA UONGOZI YAKAGUA MIRADI.

    January 16, 2025
  • Angalia Zote

Video

Baraza la Madiwani la kwanza 2020
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matumizi ya TEHAMA kwa Jiji la Tanga
  • Kata na Mitaa ya Jiji la Tanga
  • Manual ya mfumo wa FFARS
  • Muongozo wa ugawaji wa kitambulisho cha mjasiliamali
  • Jarida la Mifumo Yetu - Novemba 2018-Januari 2019
  • Kupata leseni ya Biashara
  • Tangazo kuhusu watumishi waliomba vibali vya uhamisho
  • Kuanza Ujenzi na Kupata Kibali cha Ujenzi
  • Kuhusu kupata kibali cha kusafiri nje ya nchi

Tovuti Linganifu

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Mfumo wa Kuomba Vibali vya Nje ya Nchi
  • Facebook
  • Twitter
  • Instagram
  • Tanzania Government Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Independent Avenue

    Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga

    Simu ya Mezani: 027 2643068

    Simu ya Mkononi:

    Baruapepe: info@tangacc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.