Kuna jumla ya vituo 69 vya kutolea huduma za Afya, kati ya hivyo (Serikali 37 na Visivyo vya Serikali 32). Vituo vya kutolea huduma za Afya vya Serikali ni (Hospitali ya Bombo 1, Vituo vya Afya 4, Zahanati 21, Zahanati ya taasisi za umma-majeshi na mashule). Vituo vya kutolea huduma za Afya vya Binafsi ni (Vituo vya Afya 6, Maabara 5, Kiliniki 4 na Zahanati 17).
Aidha Wilaya ya Tanga ina Maduka ya Madawa Baridi (Muhimu) 126 na Maduka ya Madawa Moto (Pharmacy) 19 na kufanya Wilaya kuwa na Maduka ya Madawa yapatayo 145.
Afya ya Kinga
Halmashauri inaendeleza jitihada katika kupambana na kudhibiti ueneaji wa magonjwa na matukio ya vifo kupitia program mbalimbali zikiwemo:.
Afya ya Tiba
Kwenye eneo hili jitihada zimeelekezwa kwenye kuimarisha na kuongeza miundombinu ili kuhudumia wagonjwa na magonjwa ambayo kinga imeshindikana. Ujenzi wa Vituo vya afya viwili vya Maere na Mabokweni, Zahanati za Kirare na Mnyanjani sambamba na ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ni sehemu ya mkakati huo.
Tiba kwa wazee
Idadi ya wakazi inayokadiriwa kufikia 15000 wenye umri wa zaidi ya miaka 60 kati yao wazee 4,506 wamebainika kutokuwa na uwezo wa kujihudumia. Wazee 4,000 kati ya hao wametambuliwa na kulipiwa CHF, juhudi zinaendelea kuwabaini 506 waliosalia.. Aidha, maeneo maalum yametengewa waganga kwenye vituo vyetu vyote vya kutolea huduma ya afya ili kuwahudumia. Huduma hii ya bure kwa wazee ilikwishazinduliwa tangu mwaka 2014 kwa Wilaya yetu ya Tanga.
Madawa ya kulevya
Wilaya yetu ni moja ya maeneo yaliyoathirika sana na madawa ya kulevya. Vijana wetu wapatao 867 wamebainika kuathirika na dawa za kulevya.
Nyumba ya Utulivu (Sober House) imefunguliwa na vijana 110 wanaendelea na tiba.
Aidha, jumla ya Tsh 5 milioni zimetengwa ili kupanua huduma kwa waathirika.
Andiko maalum limeandaliwa ili kuwasilisha kwa washiriki mbalimbali wa maendeleo ikiwamo na Wizara ya Afya, Mashirika ya DINI, Mashirika yasiyo ya Kiserikali na Taasisi Mbalimbali ili kutanua wigo wa kutolea huduma hiyo.
Ukimwi
Maambukizi ya UKIMWI kwa sasa ni 3.2% ikilinganishwa na 9.7% mwaka 2010 na hatua zinazoendelea ni pamoja na:
Elimu na Uhamasishaji wa mabadiliko ya tabia unaendela kutolewa kwa wananchi.
Huduma za wagonjwa majumbani inapatikana katika Kata zote 27 na jumla ya wagonjwa 11250 wanahudumiwa.
Wilaya inasaidia vikundi vya wajasiriamali ambapo tayari kuna vikundi vipatavyo 14 vyenye wanachama kati ya 12 - 40 vinavyosaidiwa.
Kuimarisha huduma ya kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
NA.
|
HUDUMA ZITOLEWAZO
|
JINSI ZINAVYOPATIKANA
|
1
|
Kupima afya za wananchi na kutibu wagonjwa
|
- Katika Hospitali ya Wilaya, vituo vya afya na Zahanati.
|
2
|
Kutoa chanjo za magonjwa mbalimbali
|
- Hospitali, vituo vya afya na Zahanati
- Maeneo maalum yaliyotengwa katika vijijini |
3
|
Uhamasishaji na semina za kujikianga na magonjwa mbalimbali
|
- Maeneo maalum katika kata au vijiji
- Vipeperushi na matangazo |
4
|
Usimamizi wa ujenzi wa hospitali, vituo vya afya na Zahanati.
|
- Katika kata/kijiji kulingana na mpango au ufadhili.
|
5
|
Usambazaji dawa na vifaa tiba katika vituo vya kutolea huduma za afya.
|
- Hospitali, vituo vya afya, Zahanati na maeneo maalum kipindi cha milipuko ya magonjwa
|
Halmashauri ya Jiji la Tanga lina ; Vituo vya Afya 5 (Ngamiani, Pongwe, Makorora, Mikanjuni na Duga) na Zahanati 23. Kila Kata ndani ya Halmashauri ya Jiji la Tanga kuna Zahanati au Kituo cha Afya.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.