1.0: UTANGULIZI.
Idara ya Elimu Msingi ni mojawapo kati ya Idara mbalimbali zilizopo katika Halmashauri ya Jiji Tanga. Idara hii ina vitengo vinne ambavyo vinaongozwa na Wakuu wa vitengo ambao wanamsaidia Afisa Elimu katika kutekeleza majukumu yake ya Idara ya kila siku. Vitengo hivyo ni Elimu ya watu wazima, Taaluma, Vifaa na Takwimu na Utamaduni.
Kazi na majukumu ya kila kitengo yamefafanuliwa vizuri katika taarifa hii sehemu ya vitengo vilivyopo kwenye Idara. Ikumbukwe kwamba Idara ya Elimu Msingi ni moja ya Idara kubwa katika Halmashauri ya Jiji Tanga, hivyo majukumu yake ni mtambuka ambayo yanagusa Idara nyingine kama vile, Afya, Maji, Maendeleo ya Jamii, Kilimo na Mazingira.
Idara inafanya shughuli zake kwa kufuata sheria, kanuni, miongozo na taratibu zilizowekwa na TAMISEMI na Serikali kuu kwa lengo la kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata Elimu bora itakayowawezesha kufaulu mitihani yao na kumudu maisha yao ya kila siku katika Nyanja mbalimbali. Idara ina Watumishi ambao wanaweza kutimiza malengo yaliyowekwa na Idara endapo watasimamiwa na kuwepo mazingira ya kufundishia ikiwemo miundombinu mfano, Vyumba vya Madarasa, Madawati, na Matundu ya Vyoo.
2.0: DIRA YA MWELEKEO.
Halmashauri ya Jiji Tanga imedhamiria kwamba kujenga uwezo wa kutoa huduma bora na mzuri kwa wakazi wake wote ifikapo mwaka 2020.
MWELEKEO: Halmashauri ya Jiji Tanga inachukua jukumu la kuhakikisha kuwa Jamii yote inashiriki, wake kwa waume katika kupanga na kutekeleza mipango yao ya kiuchumi na kijamii ili kuinua kipato cha mwananchi ifikapo mwaka 2020.
3.0: MALENGO YA IDARA KATIKA UTOAJI WA HUDUMA.
Katika utoaji wa huduma Idara imejiwekea malengo mbalimbali yatakayosaidia utoaji wa Elimu bora katika Shule za Msingi katika Halmashauri ya Jiji Tanga
Katika kutekeleza majukumu yake Idara inashirikiana na wadau mbalimbali wa Elimu ambao ni viongozi wa Serikali za mita, Idara na Taasisi mbalimbali zisizo za Serikali, mashirika ya dini, mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOS) CBOS na wahisani mbalimbali.
4.0: VITENGO VYA IDARA NA MAJUKUMU YAKE
Kama ilivyoelezwa katika utangulizi wa taarifa hii idara ina vitengo vinne (4) ambavyo ni.
Elimu ya Watu Wazima ambayo ndani yake kuna vitengo vidogo vitano (5) ambavyo ni vielelezo, ufundi, kilimo, Sayansi kimu na Elimu Maalum.
Taaluma, Vifaa na takwimu na Utamaduni ambacho ndani yake kuna kitengo kidogo cha michezo.
5.0: MAJUKUMU YA IDARA KWA UJUMLA
Idara ya elimu msingi ina majukumu mengi ambayo yanasaidia katika utoaji wa elimu bora, kwa ujumla malengo ya idara ni haya yafuatayo:-
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.