Wilaya imefanikiwa kuifikisha huduma ya maji kwenye maeneo ya Jiji kwa kiwango cha asilimia 96.9% ya wakazi ikilinganishwa na lengo la asilimia 90.0% lililowekwa kwa mwaka 2016. Huduma hii ya maji kwenye maeneo ya Jiji inatolewa na Mamlaka ya Maji Tanga (Tanga UWASA).
Kwa upande wa wakazi wa pembezoni mwa Jiji tumevuka lengo la asilimia 75% kwa kufikisha asilimia 76% ya wakazi wa maeneo haya.
Aidha, katika kuendeleza Jitihada za Serikali kuwafikishia huduma ya maji wakazi waishio mitaa ya pembezoni mwa Jiji, mradi wa maji wa vijiji 10 unatekelezwa katika maeneo ya Marungu, Geza, Kirare, Mwarongo, Mapojoni, Kibafuta, Ndaoya, Mleni, Chongoleani na Mpirani. Utekelezaji wa mradi huu hauendi kama ulivyopangwa kutokana na ukosefu wa fedha za kutosha na kwa wakati kulingana na mikataba iliyopo. Utekelezaji wa mradi wa maji vijiji 10 utakapo kamilika utawezesha wakazi wa Jiji la Tanga kupata huduma ya maji kwa asilimia 99.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.