•JIJI SAFI TANZANIA LAJIIMARISHA KWA UNUNUZI WA MTAMBO MPYA.
•ENG. HAMSINI AWAPA FURAHA WATOTO, ASHIRIKI UTUNZAJI WA MAZINGIRA.
Julai 10, 2025.
Katika kupunguza Changamoto ya Upungufu wa Madawati kwa Shule za Msingi, Halmashauri ya Jiji la Tanga imegawa jumla ya seti za meza na viti 500 kwa baadhi ya shule hizo ambavyo vina thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 67. Viti na meza hizo, ambavyo ni sehemu ya vingine vilivyofika kabla, havitokani na ukataji wa miti (mbao), jambo linalosaidia utunzaji wa mazingira kwa kuendelea kuipa uhai maliasili zetu.
Aidha Halmshauri hiyo imenunua Mtambo (kijiko) kwaajili ya usafi ambao umegharimu zaidi ya shilingi Milioni 200. Mtambo huo, pamoja na kazi zingine, utasaidia kusukuma takataka katika dampo la Halmashauri lililopo eneo la Mpirani, kata ya Chongoleani. Mtambo huo ni moja ya mitambo ambayo Halmashauri imejiwekea malengo ya kuinunua, kusaidia kazi mbalimbali ikiwemo ya kuendelea kulifanya Jiji la Tanga kuwa Jiji safi Tanzania.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi Mtambo pamoja na Madawati hayo Mkurugenzi wa Jiji la Tanga, Mhandisi Juma Hamsini amesema kuwa hiyo ni moja ya mipango mikakati ya Halmashauri ya Jiji la Tanga iliyojiwekea katika mwaka fedha 2025/2026.
Hata hivyo amesema kuna mikakati ya uboreshaji wa elimu ikiwemo kupitia wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na mradi wa shule bora ambao una lengo la kukuza na kuinua jitihada za walimu na wanafunzi katika kuchochea ufaulu mzuri.
Kwaupande wao walimu walionufaika na mgao huo wakaeleza umuhimu wa upatikanaji wa madawati hayo katika shule zao ikiwa ni muendelezo wa kumaliza changamoto ya ukosefu wa madawati shuleni na kuishukuru Halmashauri na kuahidi Kwenda kuvitunza ili kuleta tija katika shule zao.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.