UTEKELEZAJI WA TASAF AWAMU YA TATU – JIJI LA TANGA
Mnamo mwezi Agosti 2012, TASAF Awamu ya Tatu (MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASIKINI) ilizinduliwa ambapo utekelezaji wake utakuwa wa kipindi cha miaka kumi (10) mpaka mwaka 2022.
Utekelezaji wa Awamu hii ya TASAF unafanyika kwa vipindi viwili vya miaka mitano kwa kila kipindi.
Kwa Jiji la Tanga, Utambuzi wa kaya maskini umefanyika katika maeneo mbalimbali ya Jiji ambapo jumla ya Kaya Masikini 5,518 kutoka katika Vijiji na Mitaa 88 zilihakikiwa.
Lengo la zoezi utambuzi lilikuwa ni kuziwezesha kaya hizi zilizohakikiwa kuingia katika Mpango huu
MAFANIKIO YA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI
•Japo kuwa si kwa kiwango kiubwa sana lakini tunaweza kusema kwamba watoto wanakwenda shule na kina mama wanajitahidi kuwapeleka
watoto wao kliniki za karibu na maeneo yao ili watoto waweze kupata huduma
•Pesa wanazopata zimetumika kuwanunulia watoto sare za shule, viatu, madaftari, chakula pamoja na mahitaji mengine ya shule
•Pesa hizo pia zimetumika kuongeza mtaji kwenye miradi midogomidogo ya walengwa wa kaya maskini
CHANGAMOTO ZINAZOJITOKEZA WAKATI WA UTEKELEZAJI
•Upatikanaji hafifu wa mtandao uliounganishwa na mfumo wa epicor kwenye uandikishaji wa hati za malipo na hundi hali inayopelekea kufanya
maandalizi ya malipo kwa muda wa usiku na pia siku za mwshoni mwa wiki.
•Majina ya baadhi ya walengwa kusomeka tofauti hali iliyopelekea walengwa husika kulalamika kuwa majina yao yamekatwa.
•Baadhi ya walengwa kutokuwepo wakati wa malipo kwa sababu mbalimbali mfano kusafiri au kuumwa hali inayopelekea fedha zao kurudishwa TASAF Makao Makuu.
•Baadhi ya mitaa amabayo haimo kwenye mpango wa kunusuru kaya Maskini kudai na wao wafanyiwe utaratibu wa kuingizwa kwenye mpango.
•Baadhi ya wajumbe wa kamati ya kusimamia mradi (CMC) kutokuwa waaminifu.
Hadi kufikia malipo ya mwezi Machi – Aprili 2017, kaya 5,338 zimepokea jumla ya Tsh. 164,400,000
VIJIJI NA MITAA VILIVYO NDANI YA UTEKELEZAJI WA TASAF III - TANGA JIJI.pdf
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.