• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Staff Mail |
    • Malalamiko |
Tanga City Council
Tanga City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Tanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Ujenzi
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Usafi wa Mazingira
      • Mipangomiji na Maliasili
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jiamii na Vijana
      • Maji
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Manunuzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
    • Kata
    • Mitaa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Sekta ya Utalii
    • Sekta ya Madini
    • Sekta ya Elimu
    • Sekta ya Viwanda
    • Maeneo ya Nyumba na Makazi
    • Sekta ya Misitu na Mashamba ya Miti
    • Sekta ya Uvuvi
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Usafi na Mazingira
    • Maji
    • Ardhi na Maliasili
    • Ujenzi na Miundombinu
    • Uwezeshaji Wananchi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi, Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango Miji na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Siku za Kumuona Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi Iliyoidhinishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Kanuni
    • Fomu Mbalimbali
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Majarida
    • Taarifa za Miradi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
  • TangaTV

ZOEZI LA UHAKIKI WA VIKUNDI VYA WANAWAKE NA VIJANA LAZIDI KUPAMBA MOTO JIJINI TANGA

Imewekwa: May 30th, 2018

Imeandaliwa na Naetwe Kilango;

Mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii ustawi na vijana jijini tanga Bi; Flora Shija Maagi amekemea wanavikundi wababaishaji katika jijini Tanga, ambao hutumia ujanja ujanja katika kuonyesha shughuli za miradi ya vikundi vyao, Hayo yamejitokeza wakati zoezi la uhakiki wa vikundi vinavyotarajiwa kupatiwa mkopo wa Wanawake na vijana linaendelea jijini hapo.

 Miongoni mwa kata zilizofikiwa ni pamoja na Msambweni, Mzizima, Kirare, Mabawa, Kiomoni, Chongoleani, Nguvumali, Magaoni, Chumbageni, Ngamiani kaskazini, Duga, Majengo ambapo mkuu huyo wa idara amesema baadhi ya wanavikundi wamekua wababaishaji hasa pale wanapoamua kuonyesha miradi endelevu ya watu binafsi kwa tamaa ya kutaka kukopeshwa kiwango kikubwa cha fedha ambapo wenye miradi hiyo huridhia kwa lengo la kupata fedha hizo kupitia migongo ya wanavikundi hao.

Bi; Shija amesema atasimamia kwa weledi mkubwa zoezi hilo kwa lengo la kuhakikisha fedha hizo zinawafikia walengwa na kwa kuzingatia miongozo, Hata hivyo amesisitiza kwamba suala hilo ni la kisera na pia idara yake inatekeleza ila, Mkuu huyo wa idara amesema mifuko hii si kwaajili ya kuwanufaisha mtu mmoja mmoja ambao tayari walishafanikiwa kuendeleza miradi yao, badala yake wananchi wa hali ya chini wajiunge kwenye vikundi vya kiuchumi na kuanzisha miradi ya viwango vya saizi yao ili kuiendeleza kufikia uchumi wa kati

Akizungumza na maafisa maendeleo walioko chini yake katika ofisi za maendeleo ya jamii jijini hapo Bi; Shija  amesema kada hiyo inahitaji nidhamu ya hali ya juu, uwajibikaji na weledi katika kuleta ufanisi. Amewataka maafisa maendeleo ya jamii jijini hapo na hata duniani kote kutoifedhehesha kada kwani ni taaluma pekee mtambuka na yenye wajibu wakuwafanyia wanajamii oparesheni za akili ili kuondokana na mitazamo hasi, fikra potofu halikadhalika kuwawezesha wananchi kutambua fursa zilizopo katika maeneo yao, kuzitumia na kujiendeleza kiuchumi.

Aidha Bi; Shija amesema Halmashauri yake imetenga fedha za kutosha kwaajili ya kuvikopesha vikundi vyote  vya vijana na wanawake ambavyo vitakidhi vigezo, pia amewataka wananchi kuzingatia elimu na ushauri wanaopata toka kwa maafisa maendeleo ya jamii katika jiji hilo ili kuweza kufikia viwango vya kukopesheka.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ. March 09, 2025
  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA JIJI TANGA September 27, 2024
  • TAARIFA YA MSIBA September 18, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 26, 2024
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • TANGA: MABORESHO DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KUANZA FEB. 13, 2025

    February 04, 2025
  • MENEJIMENTI WAPONGEZWA UTEKELEZAJI MIRADI, UMALIZIAJI WA VIPORO.

    February 04, 2025
  • AFUA ZA LISHE ZAFANYA VIZURI TANGA JIJI

    January 24, 2025
  • KAMATI YA FEDHA NA UONGOZI YAKAGUA MIRADI.

    January 16, 2025
  • Angalia Zote

Video

Baraza la Madiwani la kwanza 2020
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matumizi ya TEHAMA kwa Jiji la Tanga
  • Kata na Mitaa ya Jiji la Tanga
  • Manual ya mfumo wa FFARS
  • Muongozo wa ugawaji wa kitambulisho cha mjasiliamali
  • Jarida la Mifumo Yetu - Novemba 2018-Januari 2019
  • Kupata leseni ya Biashara
  • Tangazo kuhusu watumishi waliomba vibali vya uhamisho
  • Kuanza Ujenzi na Kupata Kibali cha Ujenzi
  • Kuhusu kupata kibali cha kusafiri nje ya nchi

Tovuti Linganifu

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Mfumo wa Kuomba Vibali vya Nje ya Nchi
  • Facebook
  • Twitter
  • Instagram
  • Tanzania Government Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Independent Avenue

    Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga

    Simu ya Mezani: 027 2643068

    Simu ya Mkononi:

    Baruapepe: info@tangacc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.