Jeshi la zimamoto na uokoaji jijini Tanga limesema limejipanga katika kuhakikisha linatoa elimu kwa wananchi pamoja na taasisi zote zikiwemo shule na makampuni kuhusu kujikinga na majanga ya moto.
Hayo yamesemwa na Kamanda wa Jeshi la zimamoto na uokoaji jijini Tanga Goodluck Zelote katika kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa kikosi hicho.Aidha Kamanda Zelote amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la zimamoto pindi majanga mbali mbali yanapotokea ili waweze kupata msaada wa haraka.
Pia amesema jeshi la zimamoto na uokoaji linatoa mafunzo maalum kwa vijana ngazi ya kata ili waweze kuwasaidia pindi majanga ya moto yanapotokea katika maeneo yao.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.