• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Staff Mail |
    • Malalamiko |
Tanga City Council
Tanga City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Tanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Ujenzi
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Usafi wa Mazingira
      • Mipangomiji na Maliasili
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jiamii na Vijana
      • Maji
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Manunuzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
    • Kata
    • Mitaa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Sekta ya Utalii
    • Sekta ya Madini
    • Sekta ya Elimu
    • Sekta ya Viwanda
    • Maeneo ya Nyumba na Makazi
    • Sekta ya Misitu na Mashamba ya Miti
    • Sekta ya Uvuvi
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Usafi na Mazingira
    • Maji
    • Ardhi na Maliasili
    • Ujenzi na Miundombinu
    • Uwezeshaji Wananchi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi, Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango Miji na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Siku za Kumuona Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi Iliyoidhinishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Kanuni
    • Fomu Mbalimbali
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Majarida
    • Taarifa za Miradi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
  • TangaTV

ZIARA YA MBUNGE JIMBO LA TANGA MJINI

Imewekwa: July 15th, 2022

MHE UMMY ATOA WIKI TATU KITUO CHA AFYA TONGONI KUANZA KUTOA HUDUMA.

 “Ahadi za miradi ya Afya na Elimu aanza kuzitekeleza”.

Na.Mwajuma Ernest.

Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini Mhe Ummy Mwalimu amefanya ziara katika Kata ya Tongoni na Kirare ikiwa ni moja ya utekelezaji wa majukumu yake.

Mhe Ummy akiwa katika Kata ya Tongoni ametembelea ujenzi wa Kituo cha Afya Tongoni  ambacho ujenzi wa jengo la Wagonjwa wa nje(OPD)na jengo la maabara vimekamilika na ujenzi wa wodi ya wanawake na watoto umeanza ambapo hadi sasa kiasi cha shilingi milioni 500 kimetolewa ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Mbunge. Mhe Ummy amemwagiza  Mganga Mkuu wa Jiji kuhakikisha kituo hiki kinaanza kutoa huduma ifikapo tarehe 1/08/2022.

“Hapa naagiza kama Waziri ifikapo Agosti Mosi kituo hiki cha afya kianze kutoa huduma kwani majengo yamekamilika pamoja na miundombinu ya Maji Mganga Mkuu wa Jiji nadhani umenielewa”

Wakati huohuo Mhe Ummy ametembelea ujenzi wa nyumba ya Mwalimu katika Shule ya Sekondari Tongoni ambapo ameeleza kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa nyumba hiyo ambayo ina uwezo wa kukaa familia mbili za walimu. Mwaka 2021, Mhe Ummy alitoa ahadi ya kutafuta shilingi milioni 50 ili kujenga nyumba hiyo kwa lengo la kuboresha mazingira ya walimu baada ya kutembelea shule hiyo.

“Ahadi yangu ya ujenzi wa nyumba za waalimu naitekeleza nimeridhishwa na kasi ya ujenzi wa nyumba hii kwakweli hili litasaidia katika kuboresha elimu kwa kuwaweka waalimu karibu na shule”

Mhe Ummy pia aliendelea kusisitiza kuwa anaendelea kutafuta fedha ili shule hiyo iwe na kidato cha 5 na 6.


Aidha Mhe Ummy alikutana na wananchi na kusikiliza kero zao katika mtaa wa Tongoni, ambazo ilikuwa ni mikopo kwa wenye ulemavu, ujenzi wa zahanati Maere na ukosefu wa umeme Kiwavu. Kero nyingine ni maeneo mengi kuachwa mapori na wawekezaji na hivyo wananchi kukosa maeneo ya ujenzi.


Kuhusu swala la mikopo Mhe Ummy alimwagiza Afisa maendeleo wa kata kuhakikisha anakutana na vikundi hivyo ili awape elimu na kuwahakikishia wananchi wa Tongoni  kuwa fedha za mikopo isiyo na riba kutoka halmashauri zipo,pia amewahakikishia wananchi wa Maere kuwa anatafuta fedha za ujenzi wa zahanati ya  Maere.


Katika kata ya Kirare, Mhe Ummy alikutana na wananchi na kusikiliza kero zao ambazo ni pamoja na ubovu wa barabara na ukosefu wa umeme na alitembelea eneo ambalo wananchi wa Shaurimoyo na Kilombero wanaomba kujengewa shule shikizi ili kuwapunguzia umbali watoto wadogo wa maeneo hao.

Katika ziara hiyo Mhe Ummy aliambatana na Diwani wa kata ya Tongoni Mhe Nassoro Salimu na diwani wa kata ya Kirare Mhe Adam Mwagilo na mganga mkuu wa jiji Dr. Charles Mkombe ambapo walimpongeza Mhe Ummy na Mhe.Rais Samia Suluhu kwa kuendelea kuleta miradi mbalimbali katika jiji la Tanga.


Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ. March 09, 2025
  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA JIJI TANGA September 27, 2024
  • TAARIFA YA MSIBA September 18, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 26, 2024
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • TANGA: MABORESHO DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KUANZA FEB. 13, 2025

    February 04, 2025
  • MENEJIMENTI WAPONGEZWA UTEKELEZAJI MIRADI, UMALIZIAJI WA VIPORO.

    February 04, 2025
  • AFUA ZA LISHE ZAFANYA VIZURI TANGA JIJI

    January 24, 2025
  • KAMATI YA FEDHA NA UONGOZI YAKAGUA MIRADI.

    January 16, 2025
  • Angalia Zote

Video

Baraza la Madiwani la kwanza 2020
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matumizi ya TEHAMA kwa Jiji la Tanga
  • Kata na Mitaa ya Jiji la Tanga
  • Manual ya mfumo wa FFARS
  • Muongozo wa ugawaji wa kitambulisho cha mjasiliamali
  • Jarida la Mifumo Yetu - Novemba 2018-Januari 2019
  • Kupata leseni ya Biashara
  • Tangazo kuhusu watumishi waliomba vibali vya uhamisho
  • Kuanza Ujenzi na Kupata Kibali cha Ujenzi
  • Kuhusu kupata kibali cha kusafiri nje ya nchi

Tovuti Linganifu

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Mfumo wa Kuomba Vibali vya Nje ya Nchi
  • Facebook
  • Twitter
  • Instagram
  • Tanzania Government Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Independent Avenue

    Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga

    Simu ya Mezani: 027 2643068

    Simu ya Mkononi:

    Baruapepe: info@tangacc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.