Na: Mwajuma Ernest
Zaidi ya wanufaika elfu mbili (2000) wa mradi wa TASAF katika Jiji la Tanga, wamehitimu kupokea fedha chini ya mpango wa kuziwezesha kaya za walengwa, kwa kipindi cha miaka kumi ambacho walinufaika na mpango huo.
Akizungumza katika zoezi la malipo ya walengwa katika dirisha la 18 la mwezi Machi, lililofanyika Jumatatu, Julai 09, 2024, Afisa Ufuatiliaji wa Tasaf Jiji la Tanga, Yohana Lwendo, amesema kuwa kaya zilizokuwa zinanufaika na Tasaf tangu mwaka 2015 zilikuwa zinatambulika na tathmini ya walengwa ilifanyika mwaka Jana mwezi wa saba Ili kubaini walengwa ambao hali zao za uchumi zimekuwa bora ukilinganisha na Hali waliyokuwa nayo wakati wanaanza ambapo dodoso lilipita na kuzitambua kaya husika.
"Jumla ya walengwa 2674 wamehitimu katika dirisha la mwezi wa tatu wamepokea malipo yao na hawatakuwa wanapokea tena malipo kama ilivyokuwa kwa muda wa miaka 10 iliyopita", amesema Lwendo
Naye Mratibu wa Tasaf jiji la Tanga, Juma Mkombozi amesema kuwa wanufaika walikuwa wanajengewa uwezo kuhusu namna ya kufuata utaratibu wa mpango juu ya Matumizi ya ruzuku lakini pia namna ya kuanzisha shughuli ndogondogo za uzalishaji ili kukuza kipato cha kaya zao.
"Aidha kwa mwaka Jana tulianzisha vikundi vya kuweka na kuwekeza ambapo walengwa wanasaidika kukopeshana wao Kwa wao lakini nawasisitiza vikundi vikiimarika watapata mikopo nafuu lakini wakiitaji Elimu yoyote ya fedha ni rahisi kusaidika lakini vikundi hivi vikiimarika ni rahisi kuunganishwa na mikopo ya asilimia 10 ya Halmashauri bila riba kwahiyo wao waendelee kushirikiana kwani ni ukombozi wao" amesema Mkombozi
Nao baadhi ya wahitimu wanufaika wa Tasaf, Bi. Mwanakombo Jafari ameishukuru Serikali Kwa kuwajali Kwa kipindi chote walichokuwa wanapokea ruzuku kwani imemsaidia kusomesha watoto lakini pia kununua kiwanja .
Naye lusi John kutoka mtaa wa Gofu juu ambaye ni mhitimu wa Tasaf ameishukuru Serikali kwa kumwezesha Kwa kipindi chote Cha miaka 10 kwani ameweza kununua pikipiki.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.