Desemba 6, 2023.
Katibu Tawala Wilaya ya Tanga, na Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya maadhimisho ya Miaka 62 ya Uhuru, Wilaya ya Tanga, Ndg. Dalmia Mikaya, amewaongoza wafanyabiashara, watumishi wa umma na sekta binafsi, pamoja na wakazi wa Ngamiani katika zoezi la kufanya usafi katika Soko la Ngamiani, lililopo Kata ya Ngamiani Kati, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya juma la kuelekea siku ya Uhuru, Desemba 9.
Zoezi hilo la usafi, lililohudhuriwa pia na Diwani wa Kata hiyo, Mhe. Habib Mpa, lilihitimishwa na utoaji wa elimu ya kupiga vita vitendo vya ukatili wa kijinsia, ambapo wataalam kutoka Halmashauri na wadau wengine walitoa elimu hiyo.
Shughuli mbalimbali za maadhimisho haya zimeanza kutekelezwa tangu Desemba 2, 2023, ambapo kesho Desemba 7 kutafanyika Mashindano ya insha kwa shule za Msingi na Sekondari Wilaya ya Tanga, na Desemba 8 ikiwa ni siku ya Mashindano ya michezo kama Jogging, Mpira wa miguu (Football), Mpira wa pete (Netball), Kuvuta Kamba, Kukimbiza kuku na mingineyo.
Kilele cha maadhimisho ya miaka 62 ya uhuru wa Tanzania Bara kitakuwa Desemba 9 ambapo kutafanyika Mdahalo, utoaji wa zawadi kwa washindi wa michezo, shughuli itakayo pambwa na burudani mbalimbali.
Kauli mbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu 2023 inasema, "UMOJA NA MSHIKAMANO NI CHACHU YA MAENDELEO YA TAIFA LETU".
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.