Waziri wa Afya Wazee Jinsia na Watoto Mh Ummy Mwalimu ameipongeza Halmashauri ya Jiji la Tanga kuwezesha kukamilika kwa Zahanati ya Kwanjeka.
Mhe.Ummy Mwalimu ametoa kauli hiyo wakati akizindua Zahanati ya Kwanjeka Nyota iliyopo kata ya Mnyanjani jijini Tanga.
Aidha Mhe.Ummy Mwalimu ameziagiza Halmashauri zote Nchini kutumia Rasilimali fedha na makusanyo yao kutatua changamoto za Mwananchi ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya kutoa huduma za Afya na kusisitiza kuwa linapokuja swala la maendeleo ya wanatanga hakuna vyama.
"Uwepo wa zahanati hii ya Kwanjeka ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya kusogeza huduma za Afya karibu na wananchi kwaiyo Watendaji,Mkurugenzi,na CHMT kamati ya uwezeshaji ya Afya ya Halmashauri matarajio yangu ni kwamba kutatolewa Huduma bora za Afya naisio jengo suri tu,Hospitali na Zahanati ni huduma sio kuwa na majengo wataalam mpo mnanisikiliza ni lazima tuhakikishe vifaa vyote muhimu vinapatikana"Amesema hayo Ummy Mwalimu.
Pia amewataka watumishi watakaofanya kazi katika Hospitali hiyo ni marufuku kutoa lugha chafu kwa wagonjwa au wateja wao hivyo anamatarajio ya kuwa watatoa huduma nzuri sambamba na lugha nzuri kwa wananchi na kuwataka wananchi kutoa taarifa ya muuguzi yeyote atakayehitaji rushwa au kutoa lugha mbaya.
"Mimi ninaamini watumishi wetu wa Afya tumewapa maelekezo mazuri kwa kuzingatia kanuni,Maadili;na uweledi wa utendaji kazi zenu pia tutajitahidi kama serikali kuu kuongeza watumishi wa Afya tumeomba Utumishi watupatie kibali cha kuajiri hivyo tunaamini kabla ya mwisho wa mwaka huu tutakuwa tumeajiri watumishi kwa nafasi yangu kama Waziri wa Afya lakini pia kama mbunge kutokea Tanga mjini nitahakikisha huduma au vipimo vyote muhimu vinapatikana hapa tunamshukuru Balozi wa China ametupatia shillingi Milioni 40 kwa ajali ya kununua vifaa tiba vikiwa tayari Mkurugenzi tutakukabidhi"Amesema hayo Ummy Mwalimu
Mhe.Ummy Mwalimu amewaomba wakazi wa jiji la Tanga na Tanzania kwa ujumla kujiunga na Bima ya Afya CHF iliyoboreshwa kwa shillingi 30,000 kwa watu 6 kwa mwaka mzima na wamefanya maamuzi kama Serikali kuhakikisha kila Mtanzania hata awe masini anapata huduma ya Afya bila kikwazo cha fedha.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.