Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela amesema Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa anatarajia kufanya ziara tarehe 1 mwezi wa 6 Mkoani Tanga ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa agizo lake kwa bodi ya mkonge alilolitoa mwezi wa 3 Mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari Shigela alisema Waziri Mkuu anatarajiwa kuzindua jengo la bodi ya mkonge lililopo Jijini Tanga na baadae atatembelea Taasisi ya utafiti ya mlingano na kukagua vitalu vya zao hilo .
Shigela alisema kuwa ziara hiyo ni mahususi kwaajili ya kufuatiali maagizo aliyoyatoa tarehe 1 mwezi 3 mwaka huu baada ya kupokea taarifa ya kamati maalum aliyounda kwaajili ya kufuatilia mali za bodi ya mkonge .
“Waziri Mkuu anatarajia kufanya ziara katika Mkoa wetu na ziara hiyo itakuwa ni mwendelezo wa ziara yake aliyoifanya mwezi wa 3 na akatoa maagizo fulani kwaiyo hiyo ziara itakuwa mahususi kwaajili ya kuja kuona maagizo aliyokwisha yatoa ya ufuatiliaji na ufafanuzi wa zao la mkonge na namna ya utekelezaji na urejeshwaji wa mali ambazo zilitajwa kuwa ziliporwa kinyume cha utaratibu na sheria “Alisema Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigelas
Shigela aliendelea kufafanua kuwa ujio huo ndio utakuwa ukombozi katika Mkoa wa Tanga kwani endapo zao la mkonge litafufuliwa na kuimarishwa Mkoani humo Wananchi wataweza kujikwamua kiuchumi kutokana na kilimo cha zao hilo.
Ziara hiyo ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ina lengo la kufuatilia utekelezaji wa majengo pamoja na mashamba ya bodi ya mkonge yaliyokuwa yamechukuliwa na Wananchi kinyemela kwa maslahi yao binafsi ambapo baadhi yao hujiwekea katika Taasisi zao binafsi .
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.