Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Seleman Jaffo amefanya ziara ya kukagua miradi tisa Mkoani Tanga.
Akiwa katika ziara hiyo ya kukagua miradi Waziri Jafo ameipongeza Halmashauri ya Jiji la Tanga jinsi ilivyotekeleza miradi yake kwa ubora na kuwataka viongozi wa Mkoa wa Dar es salam kuja kujifunza katika Halmashauri hiyo .
Amesema kuwa Tanga ni Wilaya pekee Tanzania Ambayo imejenga dampo lenye ukuta mzuri ambao una ukubwa wa zaidi ya ekari 75 zote zikiwa zimetumika kujengea ukuta huo.
“ Niwapongeze kiupekee Tanga kwa kujenga dampo hili kwasababu nadir dampo pekken la Tanzania nilikopita zaaide ya ekari 75 zote mmetumia kujengea Ukuta wakisasa mko vizuri naniwatake viongozi wa Mkoa Dares salaam wake kujifunza Tanga waone ilani inavyotekelezwa vizuri katika Mkoa huu",.Alisema Seleman Jafo
Waziri Jafo ameongeza kuwa kila kiongozi amepewa dhamana ya kusimamia majukumu yake mwenyewe katika Mikoa, Wilaya na maeneo mengine hivyo kila kiongozi lazima afanye kazi yake kwa umakini na si kusubiri kusimamiwa na viongozi wangazi za juu.
“Watu wanataka kila eneo waziri ukaweke mkono nini majukumu yenu ninyi viongozi mliopewa dhamana kama viongozi wa kusimamia ? Sio kila kitu mpaka afike Rais au Makamu wa Rais au Waziri mmepewa dhamana ya kusimamia Mikoa yenu ,Wilaya zenu, na maeneo yenu kila kiongozi lazima afanye kazi yake kwa umakini”,.Alisema Waziri Jafo
Pia Mhe.Jafo alitembelea mradi wa ujenzi wa jengo jipya la Halmashauri ya Jiji la Tanga ambalo linajengwa kwa makusanyo ya Mapato ya ndani, Ukarabati wa shule ya sekondari Usagara na shule ya sekondari Galanos iliyopo kata ya Nguvumali, ujenzi wa kituo cha afya Mwakidila kilichopo kata ya Tangasisi ,Kiwanda cha ushonaji nguo cha Makorora,ujenzi wa Hospitali ya Wilaya iliyopo Masiwani ,Jengo la kitega Uchumi lililopo katika stendi ya mabasi Kange iliyopo kata ya Maweni pamoja na kiwanda cha Matofali .
Mhe . Seleman Jaffo akiwa katika eneo la dampo Jijini Tanga .
Eneo la dampo lenye zaidi ya ekari 75 lililopo Jijini Tanga .
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.