Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu na watu wenye ulemavu Stela Ikupa amewaasa wazazi na walezi wa Wilaya ya Tanga kuwapa elimu ya maisha watoto wao ili iweze kuwasaidie kujitambua.
Ikupa amesema hayo wakati wa ziara yake aliyoifanya Wilayani Tanga na kusema kuna umuhimu mkubwa kwa wazazi kukaa na watoto wao na kuwaelimisha kuhusiana na maisha kuliko kusubiri watoto wafundishwe shuleni .
“Kila mzazi achukue jukumu la kukaa na watoto wake na kuwaeleza yaliyopo ndani ya dunia na kuwambia wakienda kwa njia hii wataishia pale na wakienda kwa njia hii watafika pale itasaidia kuliko kusuburi viongozi wa dini na walimu mashuleni ,kwani msingi wa malezi bora unaanza ndani ya familia na samaki mkunje angali mbichi “,.Alisema Stela Ikupa
Sambamba na hilo Ikupa amewashauri wanasiasa wanapoelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa wawe na wakalimani wa lugha za alama ili waweze kuwasaidia watu ambao wanashida ya kusikia kwa sababu wamekuwa wakiachwa nyuma .
“Tunapoelekea katika uchaguzi tuangalie ni jinsi gani tunaweza kuwahimiza wanasiasa kuwa na wakalimani wa lugha ya alama ambao wataweza kuwasaidia watu ambao wana shida ya kusikia waweze kuelewa lakini kuwa na mkakati wa kuwa na mtu kama huyo ifike mahari tuwe na mtu kama huyo katika Halmashauri”,.Alisema Ikupa
Pia stela aliweza kutembelea kituo cha watu wenye ulemavu cha YDCP na kuwapongeza kwa kujikubali na kuwataka walemavu ambao hawajajitokeza waweze kujitokeze na kujiunga katika vikundi mbalimbali vya ujasiriamali .
Aidha Stela amewashauri walemavu hao kujitokeza na kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi na kuwachagua viongozi wa serikali za mitaa wanaowafaa s na kuacha dhana ya kuamini kuwa hawawezi kuwa viongozi .
Baadhi ya walemavu katika kituo cha YDCP kilichopo Jijini Tanga
Mkalimani wa lugha za alama akiwaelekeza wenzake
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.