Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela ametoa wito kwa wawekezaji nchini kuja kuwekeza katika fursa mbalimbali zilizopo Mkoani Tanga.
Shigela amesema hayo wakati akizungumza na Tanga Televisheni ambapo amesema kuwa Mkoa wa Tanga una fursa nyingi za Kiuchumi kwa upande wa Biashara,Kilimo na hata Madini na hivyo ni wasaa wa wawekezaji kutumia vyema wakati huu.
“Mkoa wa Tanga unasifika kwa zao la Mkonge kwa miaka nenda rudi na zao lenye bei nzuri kabisa na pia Tanga tunayo sehemu kubwa ambayo wawekezaji wanaweza kuja kuwekeza hapa kwetu “.,Alisema Martine Shigela Mkuu wa Mkoa wa Tanga
Shigela ameongeza kuwa kwa sasa wanahitaji kiwanda kitakachosaidia kusindika zao la Mkonge kwani Wakulima wa Mkoa wa Tanga wamejitahidi kulima kwa hali na mali .
“Tukipata Mashine au Kiwanda cha Usindikaji kitasaidia sana Wakulima wetu kuzalisha kwa wingi zaidi na kusafirisha kwa haraka bidhaa zao “.,Alisema Mkuu wa Mkoa wa Tanga
Sambamba na hayo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela amesema katika upande wa Bomba la Mafuta bado wanaendelea na hatua mbalimbali kwani itasaidia kutoa ajila kwa wananchi wa Mkoa wa Tanga .
Mkoa wa Tanga ni moja kati ya Mikoa inayozalisha zao la mkonge kwa kiwango cha asilimia kubwa ambao unaweza kutoa ajira kwa Wananchi wa Mkoa wa Tanga .
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela akizungumza na mwandishi wa Tanga tv juu ya uwekezaji
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.