Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Daudi Mayeji amesema bandari ya Tanga imeanza kuchimba ili kupata kina kitakachosaidia meri za mizigo ziweze kushusha katika bandari hiyo.
Mayeji amesema hayo katika ziara ya Wawakilishi wa Bunge kutoka visiwani Zanzibar waliofanya ziara Jijini Tanga lengo likiwa ni kujifunza mambo mbalimbali kutoka Jijini hapo .
Amesema lengo la kuitengeneza bandari hiyo ni kuwasaidia wafanya biashara kutoka visiwani kuja na mizigo yao ili kukuza soko la biashara ya Jiji hilo .
“tunavyozungumza bandari ya Tanga meri imeanza kuchimba ili kupata kina chenye kilomita 15 ambayo iliyopo ina kilomita 4.5 ambayo inasababisha meri za mizigo zisiweze kufunga nanga katika bandari ya jiji hilo ambapo tunategemea mwaka huu ukarabati utakapokuwa umekamilika meri kubwa za mizigo zitaanza kufunga hapa “,.Alisema Daudi Mayeji Mkurugenzi wa Jiji la Tanga
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Ustawi wa jamii kutoka visiwani Zanzibar Mwanaasha Juma amewaasa wazazi kujenga mahusiano mazuri na walimu ili waweze kuwasaidia watoto wao kitaaluma.
Mwanaasha amesema hayo wakati walipotembelea shule ya Pongwe na Majani mapana zenye watoto wenye mahitaji maalum zilizopo Jijini Tanga .
“Ni vizuri wazazi wa watoto hawa kutengeneza mazoea na ushirikiano mzuri na walimu ili linapotokea tatizo kwa mototo kwa sababu ya ule mushikamano baina ya mzazi na mwalimu tunaweza kumsaidia motto huyu kuwa vizuri katika taaluma”,.
Lengo kuu la ziara ya wawakilishi hao ni kuja kujifunza mambo mbalimbali Jijini Tanga ambapo waliweza kutembelea shule ya sekondari ya Tanga ufundi,Mkwakwani sekondari ,Hospitali ya Wilaya ,Dampo na walihitimisha ziara yao kwa kutembelea kituo cha matangazo cha Tanga television.
Wawakilishi wa bunge kutoka Zanzibar wakiwa na wanafunzi wa shule ya msingi pongwe
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.