Mkuu wa Wilaya Tanga Thobias Mwilapwa amewapongeza wananchi wa Jiji hilo ambao wamejitokeza kwa wingi kupima chanjo ya magonjwa surua pamoja na rubella.
Mwilapwa ametoa pongezi hizo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya chanjo dhidi ya surua na rubella kwa watoto wenye umri chini ya miaka 5 iliyofanyika katika kituo cha afya cha Ngamiani kilichopo Jijini tanga ambapo wananchi wameonesha mwitikio mkubwa ikiwa ni siku ya kwanza ya kuanza zoezi hilo .
Mwilapwa ameongeza kuwa Taifa limeanzisha kampeni ya kupambana na magonjwa matatu ambapo kati ya magonjwa hayo mawili yanafanana ambayo ni surua na rubella pamoja na polio .
“Taifa letu limeanzisha kampeni ya namna hii ya kupambana na magonjwa matatu ambayo mawili yanafanana sana surua na rubella pamoja na polio tangu mwaka 1999 na kila baada ya miaka 3tunafanya kitendo cha kampeni yenye lengo la kuhamasisha ufahamu kwa watu wengi kuhusu mambo ya msingi na mambo yanayotakiwa kufanyika “,.Alisema Thobias Mwilapwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga
Pia Mwilapwa ameongeza kuwa serikali inatumia fedha kwaajili ya kusaidia wananchi wake hivyo wanapaswa kujitokeza zaidi ili kupima na kutambua afya za watoto wao na kupewa chanjo .
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Jonathan Budenu amesema lengo kuu la kampeni hiyo ni kupambana na kuzuia na magojwa yanayoweza kuzuilika na chanjo .
“Tunazuia magonjwa haya kwa kutoa chanjo kwa watoto wote wenye umri kati ya miezi 9 hadi chini ya miaka 5 na kampeni hiyo itafanyika katika vituo vyote vya afya pamoja na maeneo ambayo yatakuwa yamechaguliwa kuweza kuwasogezea wananchi huduma hii karibu”,.Alisema Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga
Kauli mbiu ya kampeni ya chanzo dhidi ya surua na rubella kwa watoto wenye umri chini ya miaka 5 ni Chanzo ni kinga kwa pamoja tuwakinge .
Wananchi wakiwa katika kituo cha Ngamiani kuwapima watoto wao surua na rubella Jijini Tanga
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Jonathan Budenu akiwaasa wananchi kujitokeza ili kuwapa watoto wao chanjo
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.