Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe Ummy Mwalimu leo tarehe 26/4/2021 amekabidhi hundi ya milioni 300 kwa vikundi 37 vya wanawake, watu wenye walemavu na vijana kutoka kata 17 za jiji la Tanga ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi wa Serikali ya awamu ya sita.
Lengo la mikopo hiyo ni kuhakikisha kuwa wananchi wanapata mikopo isiyo na riba na hivyo kuepuka mikopo kandamizi yenye riba kubwa ambayo inawaingiza katika umasikini.
Akizungumza wakati wa kukabidhi mikopo hiyo, Mhe Ummy ameipongeza Halmashauri ya Jiji la kwa kuzingatia vyema maelekezo ya Serikali ya kutoa mikopo hii ambapo katika mwaka huu wa fedha 2020/21 wametoa kiasi cha shilingi milioni 994 sawa na asilimia 81 ya lengo. Mhe Ummy amewataka wanufaika wa mikopo hii kuzitumia fedha walizopewa kwa kusudi lililolengwa ambalo ni kufanya shughuli za kujiongezea vipato na sio vinginevyo.
Kwa Upande wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Tanga Daudi Mayeji amesema ataendelea kuhakikisha idara ya Maendeleo ya Jamii wanatoa elimu kwa vikundi kabla na baada ya kupata mikopo hiyo .
Makabidhiano ya mikopo hiyo imehudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martin Shigella, Naibu katibu Mkuu OR TAMISEMI anaeshughulikia Afya na Maendeleo ya Jamii, Dr.Grace Maghembe, Mkuu wa wilaya wa Tanga Mhe Tobias Mwilapwa, Mstahiki Meya wa Jiji la Mhe. Abdulahaman Shiloow, Kamati ya Fedha Jijini Tanga na viongozi na wataalam mbalimbali.
Mhe.Ummy Mwalimu akiongea na Wananchi waliohudhuria hafla ya utoaji Mikopo.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.