Baadhi ya kinamama Jijini Tanga wameungana na kusaidia kazi ya ujenzi inayoendelea katika shule ya sekondari ya masechu iliyopo kata ya Chumbageni Jijini Tanga kwa lengo la kuunga mkono Juhudi za serikali za kutoa elimu bure.
Wakiwa katika shule hiyo Diwani wa kata hiyo Saida Gadaf amewashukuru wanawake hao kwa kuwa na umoja na mshikamano katika kufanisha jambo hilo.
"Awali ya yote nianze kumshukuru mwenyezi mungu kwa kukamilisha zoezi hili siku ambayo dunia inatambua tumekutana hapa wanawake ili tuweze kufanya kazi tunaona ufaulu wa wanafunzi mashuleni umeongezeka na ndio maana tumeamua kujaribu kufanya kitu",.Alisema Diwani wa kata ya Chumbageni
Kwa upande wa baadhi ya viongozi kutoka ngazi mbalimbali ambao wameshiriki katika zoezi hilo wameeleza jinsi walivyotekeleza kila walichokubaliana .
"Tumeanza mbali kwa kuanzia vikao mbalimbali na tumeshikana mikono na kufanikisha kuleta vile tulivyokusudia kulifanya ",.Walisema baadhi ya viongozi
Nao wananchi wa Jiji la Tanga wameeleza jinsi walivyopendezwa na tukio hilo na kuwasifu viongozi hao kwa jambo hilo.
Sambamba na hayo pia amewataka kinamama wenzao kuwa na umoja pindi yanapotokea mambo ya kushirikiana ili kusaidia watoto wao kupata elimu bora .
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.