Afisa tawala wa Mkoa wa Tanga Judica Omary amewataka wanawake wa Mkoa wa Tanga kujumuika pamoja kuvifichua vitendo vya kikatili ili kuweza kutokomeza Vitendo hivyo .
Afisa tawala huyo ameyasema hayo katika kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika katika uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
"Siku hii ya leo inatupa nafasi ya kuelimishana umuhimu wa kujua usawa wa kijinsia na kuongeza ushiriki wa wanawake katika uongozi pamoja na utengenezaji wa maadhimisho mbalimbali Pamoja na kuibua vitendo vya ukatili wa kijinsia",.Alisema Afisa Tawala Mkoa wa Tanga Judica Omary
Pia amewakumbusha wanawake hao kujua changamoto ambazo zimekuwa zikiwakabili wanawake pamoja na Vijana na kuangalia ni jinsi gani ya kuzitatua.
Afisa tawala ameongezea kuwa wanawake wanatakiwa kuondoa uwezo mdogo wa wanawake katika kusoma na kuandika na katika masuala mazima ya elimu kwani maadhimisho hayo yanagusa juu ya kuwa na haki za kiafya.,elimu na kufanya maamuzi sahihi.
Kwa upande wake Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii Jiji la Tanga Omary Ally ameeleza jinsi Halmashauri ya Jiji la Tanga inavyowashirikisha wanawake katika mipango mbalimbali kama utoaji wa mikopo kwa wanawake.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.