Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela amepokea msaada wa ndoo 85 za koki kutoka Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira TANGAUWASA ili kuwawezesha watu kunawa mikono yao mara kwa mara kwa kutumia maji tiririka kwenye maeneo ya masoko ,Vituo vya Stendi ya mabasi na Hospitali Wilaya ya Pangani ,Tanga Jiji pamoja na Muheza .
Akipokea vifaa hivyo Martine Shigela alisema vifaa hivyo vitatumika kwaajili ya kunawa mikono nakuendelea kujikinga na magonjwa ya milipuko .
“Niwapongeze sana mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Jiji la Tanga kwani vifaa hivi vitatumika katika kukabiliana na magonjwa ya milipuko kwasababu corona sasa hamna tena “Alisema Mkuu Mkoa wa Tanga Martine Shigela
Shigela aliongeza kwa kumtaka Mwenyekiti wa Halmashauri ya Jiji la Tanga kuhakikisha vifaa hivyo vilivyotolewa na Mamlaka ya maji vinatumika vizuri katika maeneo vitakapopelekwa .
Kwaupande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Maji safi na usafi wa mazingira TANGAUWASA Geofrey Hilly alisema msaada huo ni kwa lengo la kusaidia juhudi ya Serikali kukabiliana na ugonjwa wa COVID 19 Mkoani Tanga
Vifaa vilivyotolewa na Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira TANGAUWASA ni ndoo 85 ambazo zitagawanywa katika Kituo cha afya cha Duga ,Ngamiani ,Mikanjuni ,Pongwe ,Msoko ya Mgandini ,Mlango wa chuma ,Deep sea,Kasera ,Kange stendi,Ofisi kuu ya Jiji ,Depot pamoja na Mipangomiji .
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.