Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mustafa Selebosi amewataka Viongozi katika ngazi za Mitaa kuwahimiza Wananchi katika kuchangia Maendeleo katika Mitaa yao.
Selebosi ameyasema hayo wakati wa hafla ya kupoke msaada wa vitanda ,Magodoro na Mashuka katika kitua cha Afya Duga kutoka kiwanda cha vipodozi (Tanga Pharmaceutical and plastic limited) TPPL kilichopo Mkoani Tanga
Akizungumza na Viongozi wa Mtaa wa Duga ikiwemo Diwani,Watendaji , Wenyeviti pamoja na Wahudumu wa Afya wa Kituo cha Afya Duga Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mustafa Seleboss amesema kuwa ni vema Viongozi wa Mitaa wakawahimiza Wananchi wao kuchangia Maendeleo katika Mitaa wanayoishi ili kuunga jitihada za Serikali katika utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo.
Sambaba na hayo Selebosi amesema kuwa atashirikiana na Viongozi wa Kata ya Duga katika kujenga uzio wa kituo hicho cha Afya ili kulinda usalama wa eneo hilo.
“ Lakini kingine niwaombe Wenyeviti Mhe Diwani amezungumza kuhusu suala la uzio tunatakiwa tuangalie huduma za kijamii kwanza kuhamasisha Wananchi chini ya Mhe Diwani kweza kuchangia Maendeleo katika eneo hili na ni wajibu wetu kuimarisha vituo hivi ili kupunguza msongamano uliopo ndani ya eneo hili ” ,.Alisema Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mustapha Seleboss
kwa upande wake Diwani waKkata ya Duga Khalid Rashidi amewapongeza watoa huduma wa Kituo hicho cha Afya kwa kuwahudumia Wananchi wa Kata ya Duga na Kata za jirani huku Mwenyekiti wa CCM Kata ya Duga Joseph Kilumbo ameeleza namna Chama hicho kinavyotekelza ilani yake.
Nae Mganga Mfawidi wa Kituo cha Afya cha Duga Dkt Magreth Matutu ameeleza taarifa ya kituo huku Mwenyekiti wa kamati ya huduma za jamii Shiloo ametoa wito kwa Mashirika mengine kuweza kusaidia na kuunga mkono jitihada za Serikali.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.