Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambaye ni MKuu wa Wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa amewataka wakazi wa Jiji la Tanga kushirikiana na Vyombo vya Usalama kwa Kutoa taarifa juu ya uwepo wa viashiria vya uharifu ili kuendeleza amani iliyopo katika Jiji hilo.
Mwilapwa amesema hayo wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Tanga baada ya kuibuka kwa kikundi kinachotajwa kufanya uhalifu katika Maeneo mbalimbali ya Jiji hilo.
Mwilapwa amesema kuwa siku za hivi Karibuni kumekuwa na Matukio ya Uharifu katika Jiji la Tanga ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa tukio la kuvamiwa kwa mwenyekiti wa Mtaa wa Railways kata ya Centreal na kisha kuchomwa na kitu chenye ncha kali.
“Madhara ya uharifu hayachagui mtu jambo la kusikitisha kabisa mmoja wa viongozi wetu tuliyemwapisha tarehe 25/11/2019 ambaye ni mwenyekiti wa mtaa alivamiwa na kuchomwa na kitu chenye ncha kali shingoni lakini tusiwe na hofu kwakuwa Serikali yetu ipo kazini vyombo vya usalama vipo imara wananchi ondoeni shaka “,.Alisema MKuu wa Wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga amewasisitiza viongozi na kuwataka madiwani kushirikiana na viongozi wa kata ili kuweza kutokomeza vitendo hivyo .
“Niwaombe viongozi kama alivyosisitiza Mkuu wa Wilaya sisi sote ni Viongozi naamini vibaka hawa wameongezeka kwa lengo kuu la kutaka kuzoofisha nguvu ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli ile ya kuwaachia huru wale wafungwa ili ionekane kwamba wale wafungwa ni sehemu ya kuongezeka kwa uharifu na mimi naamini Mhe Rais anania njema yakupunguza idadi ya wafungwa gerezani kwa lengo la kuwataka waje kufanya kazi za kuongeza pato la Taifa “,. Alisema Mustahiki Meya wa Jiji la Tanga Mustapha Seleboss
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Hamis Mkoba amewapongeza viongozi wa Halmashauri wa Jiji la Tanga kwa jinsi wanavyoonesha upendo katika kuliendesha baraza la Madiwani .
Lengo kuu la Baraza hilo ni kusaidiana katika yale maadhimio yaliyopitishwa na kamati mbalimbali kwa maslahi ya watu wa Jiji la Tanga.
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mustapha Seleboss akiwasisitiza Madiwani kushirikiana na viongozi wa kata kufichua waharifu.
Viongozi mbalimbali wa Jiji la Tanga wakiwa katika Baraza kujadili maadhimio yaliyopitiswa na kamati mbalimbali .
Mkuu wa Wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akiwa na Mstahiki Meya Mustapha Seleboss pamoja na Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji wakiwa katika kikao cha Baraza la Madiwani.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.