Wananchi Wa Jiji la Tanga wameshauriwa kushirikiana vyema na viongozi wa Halmashauri ya Jiji hilo katika kudumisha usafi wa mazingira na kuacha kuwa na dhana potofu kuwa manispaa na mabaraza ya Jiji ndio wanatakiwa kufanya hivyo .
Hayo yamesema na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa chakechake kutoka visiwani Zanzibar Salma Hamad wakati wa ziara yao waliyoifanya jijini Tanga ambapo amesema endapo wananchi watashirikiana katika kutunza mazingira na kuyaweka katika hali ya usafi Tanga itapiga hatua kubwa katika maendeleo .
“Bila kukusanya mapato huwezi kuendeleza miradi ya maendeleo wala huwezi kudumisha usafi wa mazingira lakini tukikubaliana kwa pamoja na tukaona hili nilakwetu kiujumla itakuwa kila siku tunapiga hatua kwaajili ya kuyaendeleza haya lakini sisi manispaa pamoja na mabaraza tutazidi kuhakikisha huduma kwa wananchi zinapatikana kwa urahisi “,.alisema Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Chakechake kutoka visiwani Zanzibar
Kwa upande wake Diwani wa Mji wa Chakechake kutoka visiwani Zanzibar Ally Yussufu ameishukuru Halmashauri ya Jiji la Tanga kwa mapokezi mazuri waliyowaonyesha nana kuwapongeza kwa jinsi wanavyotekeleza miradi ya maendeleo .
“Tunashukuru sana kwa mapokezi mazuri mliotuonesha lakini pia nimshukuru sana Afisa Mahusiano wa Jiji la Tanga kwani tumekuwa nae toka asubuhi mpaka sasa saa 12 hachoki na nimtendaji mkubwa kazini “,.Alisema Ally Yussufu Diwani kutoka Zanzibar
Nae Mohamed Ally ambaye ni Daktari kutoka Visiwani Zanzibar amesema wamejifunza vitu vingi ambavyo wanaahidi kwenda kuvifanya pindi watakaporejea Zanzibar .
wawakilishi hao waliweza kufanya ziara katika miradi mbalimbali ikiwemo Kituo cha matangazo ya runinga cha Tanga tv,Dampo,duka la dawa la Halmashauri ,Shule ya sekondari ya Usagara,kituo cha afya Ngamiani ,kiwanda cha matofali pamoja na stendi ya Kange na Lengo kuu la ziara hiyo ni kuja kujifunza mambo mbalimbali ya kimaendeleo kutoka Jijini Tanga
Kiwanda cha matofali kilichopo Jijini Tanga
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.