Mstahiki Meya wa Jiji La Tanga Mustapha Seleboss amewataka Wanafunzi kuweka juhudi katika kusoma masomo ya Sayansi ili kuwa wajuzi na kuingia katika soko la dunia kwa kupitia masomo hayo .
Seleboss amesema hayo wakati wa sherehe za wiki ya Sayansi Afrika ambayo imejumuisha Nchi 32 za Afrika naTanzania ikiwa inafanyika katika Mikoa ya Dar es salaam ,Tanga na kumalizika katika Mkoa wa Arusha.
“Daktari ni moja ya sifa inayotokana na Sayansi tunaamini Daktari ni bigwa wa masomo hayo kwaiyo leo mnaandika historia kubwa kwakuwa mmehudhuria sherehe za kuazimisha wiki ya Sayansi Afrika lazima mkumbuke kuwa mmepewa heshima kubwa kwakuwa kuna wanafunzi wengi hapa Tanga lakini umechukuliwa wewe lazima kile ulichoitiwa leo ukiweke katika kichwa chako na ili tusimwangushe daktari lazima tuwe wa kwanza katika masomo ya sayansi kwa Mkoa wa Tanga “,.Alisema Mustapha Seleboss
Sambamba na hayo Seleboss amewapongeza madaktari hao kwa kuanzisha mafunzo hayo kwa vitendo kwani yatawasaidia wanafunzi kujua vitu mbalimbali kwa urahisi zaidi .
Lwidiko Edward ni Balozi wa Next Einstein Forum Nchini Tanzania amewashukuru Viongozi wa Mkoa wa Tanga kwa mapokezi waliowaonesha na kusema kuwa lengo kuu la wiki Sayansi Afrika ni kuwafanya wanafunzi kuijua sanyansi wakiwa na umri mdogo na kuachana na dhana ya kusema Sayansi ni ngumu .
“Hili ni Baraza ambalo limejikita kuhakikisha Elimu ya Sayansi inapewa kipaumbele kwa Afrika na kuhakikisha vijana tangu umri mdogo wanaijua elimu hii “,.Alisema Lwidiko Edward ni Balozi wa Next Einstein Forum Nchini Tanzania
Maadhimisho ya wiki ya Sayansi Afrika kwa Mkoa wa Tanga yamefanyika hii leo ya tarehe 4/12/2019 katika shule ya Msingi Changa ambapo yalianzia katika Mkoa wa Dar es Salaam 3/12/2019 na yanatarajia kumalizika katika Mkoa wa Arusha tarehe 6/12/2019 .
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.