Jumla ya wanafuzi 5948 wa kidato cha nne Jijini Tanga wanatarajia kufanya mitihani yao siku ya jumatatu November 4 ya kuhitimu elimu ya sekondari kwa mwaka 2019 .
Hayo yamesemwa na Afisa elimu sekondari Jijini Tanga Lusajo Gwakisa wakati akizungumza na tanga television amesemamtihani wa Taifa kwa kidato cha nne utaanza tarehe 4 na kumalizika tarehe 22 ya mwezi 11 kwa mwaka 2019.
Pia Gwakisa amesema maaandalizi ya mitihani hiyo yako vizuri kwani wamefanya maandalizi ya kutosha kuanzia kwa wanafunzi ,madarasa pamoja na kamati ya usimamizi.
“Tutakuwa na mitihani ya taifa miwili tutakuwa na mtihani wa taifa wa kidato cha nne ambao utaanza tarehe 4 mpaka 22 na pia tutakua na mtihani wa taifa wa kitacho cha pili ambao utaanza tarehe 11mpaka tarehe 22”,.Alisema Lusajo Gwakisa Afisa Elimu Sekondari Jijini Tanga
Sambamba na hayo Gwakisa ametaja jumla ya wanafunzi wa kidato cha pili ambao wanatarajia kufanya mtihani kuwa ni wanafunzi 6200 wakiwamo wasichana 3050 na wavulana 3150.
Sanjari na hayo Gwakisa amewaasa wazazi pamoja na wanafunzi wa Jiji hilo kutojihusisha na vitendo vya udanganyifu kwani mitihani hiyo inaendeshwa kwa kanuni na taratibu za mitihani.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.