Halmashauri ya Jiji la Tanga imesema inaendelea kutoa elimu kwa wadau mbalimbali juu ya kupambana na maambukizi ya virusi hatari vya Corona.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa wakati akitoa elimu kwa wamiliki wa mabasi na kuwataka kufuata maelekezo yanayotolewa na wahudumu wa afya ili kuwalinda abiria wao.
"Tulichokuwa tumekusudia tumekipata tumefanikiwa kwani tulitaka tuelewane katika mambo ya msingi kwamaana wote tuwe tunafanya kitu kimoja mawazo yetu na yenu yawe yanafanana ili kuweza kudhibiti janga hili"Alisema Mkuu wa Wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mustapha Seleboss amesema jambo la msingi la kutiisha kikao hicho ni kuweka mikakati ya kuweza kuwalinda abiria Kwani Serikali inataka kuwalinda raia wake .
"Serikali bado inahuruma sana na wananchi wake sisi kama viongozi wa Tanga na pia wanatanga tuangalie ni namba gani tunaweza kuwasaidia wananchi wetu na tuangalie na kuhakikisha vipimo vile vinaanza kufanya kazi mapema ",.Alisema Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mustapha Seleboss
Naye mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji ameitaka sekta ya usafirishaji kuchukua hatua mapema za kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona kwani sekta hiyo ndio hubeba watu wangu.
"Ninyi ndio mabega watu wangu bila kujua wale waliopata maambukizi na wasiopata bila kujua kwahiyo tukidhibiti kwenye upande wa usafirishaji tutakuwa tumesaodia sana", .Alisema Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga
Nao wamiliki wa mabasi akiwamo Mwenyekiti wa Tarenia wameahidi kuwa makini katika huduma zao wanazozitoa ili kuweza kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.