Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (Tanzania Food and Drugs Authority – TFDA) jijini Tanga, leo imetoa mafunzo maalum kwa wajasiriamali kuhusu taratibu za ufungashaji wa bidhaa zao husan chakula.
Akilieleza lengo la mafunzo hayo ambayo yamefanyika kwenye Ukumbi wa Community Centre Tangamano Jijini Tanga, Afisa Mfawidhi wa Mamlaka hiyo Robeta Feruzi alisema, lengo kubwa ni kuwainua wajasiriamali kwenye bidhaa zao na kufahamu kanuni za moja kwa moja
Aidha kwa upande wa mkufunzi wa semina hiyo Abdallah Mkanza ameeleza kuwa wajasiriamali wanapaswa kufahamu matakwa ya kisheria pamoja na kulinda afya ya jamii kwa kuzuia adhari zinazoweza kujitokeza.
VIDEO: Abdallah Mkanza akiongea na Waandishi wa Habari
Kwa upande wa Kaimu Mkurugunzi wa Jiji la Tanga ambaye ni Mganga Mkuu wa Jiji la Tanga Dk. Jerry Khanga ameishukuru TFDA kwa kuweza kuwapatia elimu wajasiriamali wa jiji hilo juu ya taratibu za wao kupata vibali.
VIDEO: Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Tanga ambaye ni Mganga Mkuu wa Jiji la Tanga akitoa shukrani
Kwa upande wa wajasiriamali walioshiriki mafunzo hayo, nao wameishukuru TFDA kwa kuwapa elimu juu ya kudhibiti ubora, usalama wa chakula na dawa, vipodozi na vifaa tiba.
TFDA ni taasisi iliyo chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto yenye jukumu la kuthibiti ubora, usalama na ufanisi wa chakula dawa, vipodozi na vifaa tiba. Kulinda afya ya jamii kwa kuzuia athari zinazoweza kujitokeza kutokana na matumizi ya chakula, dawa vipodozi na vifaa tiba.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.