Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amewataka watumishi wa hospitali na vituo vya afya kuwa na lugha nzuri wakati wakiwahudumia Wananchi wao kwani Serikali ya awamu ya tano imeboresha huduma za afya kote Nchini .
Waziri Ummy amesema hayo wakati alipokuwa akizungumza na watumishi katika kituo cha afya Mikanjuni pamoja na Wananchi wa eneo hilo ambapo amesema katika Jiji la Tanga huduma za afya zimeboreshwa kwa asilimia kubwa .
“Tunapopima kuna viashilia vikuu na kupata takwimu sahihi ili kujua tunaenda mbele au hatuendi mbele kwaiyo watumishi wa afya lazima tutumie lugha nzuri kwani lugha za matusi dharau na kejeli havihitajiki katika kazi ,.”Alisema Ummy Mwalimu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinisa wazee na watoto
Sambamba na hayo pia alitoa wito kwa Mkurugenzi kufanyia kazi huduma za matibabu ya Wazee ili waweze kupatiwa huduma bure katika vituo vya afya pamoja na kuthaminiwa .
Mbali na hayo alitoa pongezi kwa wahudumu wa afya kwa kasi ya kutoa huduma wanayoifanya katika kupambana na ugonjwa wa Corona kwani walikuwa mstari wa mbele katika kupambana na ugonjwa huo .
Mwisho alifurahishwa na baadhi ya vituo vya afya kikiwamo cha Mikanjuni ,Makorora pamoja na kituo cha afya cha Ngamiani kwa kuanza kutoa huduma ya upasuaji wa dharura katika Jiji la Tanga .
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.