Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga, Mustafa Seleboss amewataka Waheshimiwa Madiwani kutoingilia shughuli ya watendaji wa Halmashauri wa Jiji hilo na badala yake wawasaidie kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi. Amesema hayo leo kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani kilifanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Jiji hilo.
“Waheshimiwa madiwani wenzangu, tafadhalini msiingilie shughuli za watendaji wetu, kama watendaji wamekuja kufanya kazi kwenye kata yako wape ushirikiano, lakini isiwe wewe ndio unakuwa kikwazo kisa eti wananchi hao ni wapiga kura wako wasisumbuliwe; hiyo hapana. Kama kuna shida ya kuelimishana wewe kama wahesimiwa madiwani, muwasaidie watendaji hawa” alisema Meya huyo.
Yamesemwa hayo kutokana na baadhi ya Waheshimiwa Madiwani kuwatetea wananchi wao pale wanapotakiwa kulipia tozo za huduma, hasa za uzoaji wa taka ngumu. Baadhi ya wananchi wamekuwa wakikwepa kulipia tozo za huduma ya usafi, hivyo kupelekea watendaji kuwafuatilia na kuwataka kulipia tozo za huduma hiyo, hapo ndipo kunapapotokea baadhi ya Waheshimiwa Madiwani kuingilia kati na kuwataka wananchi hao wasilipie huduma kwa sababu mbalimbali.
Kwa upande wa Waheshimiwa Madiwani nao walitoa ushauri wa namna nzuri ya kukusanya tozo hizo pamoja na uboreshaji wa huduma ili kuondoa hali ambayo imekuwa ikijitokeza baina ya wananchi na watendaji hao wakati wa kukusanya tozo hizo. Mkurugenzi wa Jiji la Tanga, ambaye ndiye msimamizi wa shughuli za Jiji hilo amepokea ushauri huo na kuahidi kuendelea kutoa huduma kwa wananchi bila ya kukwazana.
Halmashauri ya Jiji linatoa huduma ya usafi wa mazingira, ikiwa ni pamoja na kuzoa takataka kutoka kwenye kaya, maduka, migahawa, hoteli na maeneo ya soko ndani ya jiji hilo. Huduma hii huwa inalipiwa kwa mwezi kulingana na sehemu husika.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.