Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa amefungua Mradi wa huduma ya kuchuga damu katika Hospitali ya rufaa ya Bombo Katika Mkoa wa Tanga na kupunguza gharama ya Kuwasafilisha wagonjwa wenye matatizo ya figo kwenda Katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kufuata huduma hiyo.
Waziri Mkuu amefanya ufunguzi huo wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Tanga huku akisema sekta ya afya imepiga hatua kubwa kwa sasa ukilinganisha na miaka ya nyuma kwani Serikali inaendelea kuboresha huduma za afya.
"Mpango huu ni kwa hospitali zote za rufaa za kanda na sasa tunashuka kwenye Mikoa na baada ya hapo tukiona kwenye Mikoa tumeweza tutaangalia nini kiendelee kwasababu huduma zinazotolewa katika Hospitali za Wilaya zinafanana na zinazotelewa kwenye Hospitali za Mikoa",.Alisema Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa
Sambamba na hayo pia amewakumbusha wananchi wa Mkoa wa Tanga kujua umuhimu wa kujikinga na magonjwa yanayoambukizwa na yasiyoambukizwa.
Kwa upande wake Waziri wa Afya maendeleo ya jamii jinsia Wazee na watoto Ummy Mwalimu amesema awali huduma za Figo zilikuwa zinatolewa katika vituo 19 vya binafsi na Hospitali tano za Serikali .
"Serikali iliahidi kuwa itasogeza huduma za afya karibu na Wananchi na tunafanya hivyo huu Mradi tutautekeleza katika Mikoa 8 asilimia kubwa ya kusafisha damu zilikuwa zinafanywa na Hospitali binafsi pekee",.Alisema Waziri wa Afya maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Ummy Mwalimu
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa yupo Mkoani Tanga kwa ziara ya kikazi ya siku 7 ambapo atatembelea Halmashauri zote za Mkoa wa Tanga .
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.