Mkuu wa Wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa amewataka wafanyabiashara Jijini Tanga kutopandisha bei za vifaa vya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa korona .
Mwilapwa amesema hayo wakati alipotembelea wafanyabiasha na kuangalia bei elekezi ya vifaa vya kujikinga na maambukizi ya corona kama barakoa na ndoo za kuwweka maji.
“vipo vifaa ambavyo katika kukabiliana na ugonjwa wa corona vinaweza vikasaidia sana katika kukabiliana na maambukizi vifaa hivyo vinatakiwa vipatikane kwa bei halali tena ikiwezekana kwa bei rahisi tukikuta mtu kapandisha bei tutamchukulia huyo kama ni mtu ambaye anataka kulihatarisha Taifa letu atakuwa anaenda kinyume na jitihada za Serikali”,.Alisema Mkuu wa Wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
Mwilapwa ameongeza kwa kusema kuwa katika Taasisi zote za Serikali na Taasisi za Umma zimechukuliwa tahadhari mapema kwa kuweka vifaa kama ndoo za kunawia mikono .
Sambamba na hayo pia Mwilapwa amewataka Madereva pamoja na Makonda kupakia abiria katika siti na kuacha tabia ya kujaza abiria katika daladala na katika mabasi yanayokwenda Mikoani.
Hayo yanakuja baada ya Waziri wa Afya maendeleo ya Jamii jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu kutangaza kupatikana kwa wagonjwa 3 hapa Nchini .
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.