Mkuu wa Wilaya ya Tanga Thobiasi Mwilapwa amewataka wachungaji ,mapadri pamoja na mashehe kuendelea kuelimisha watu namna ya kujikinga ugonjwa na corona kwa kufanya usafi katika maeneo yao wanayoishi na katika nyumba za ibara.
Mwilapwa ameyasema hayo wakati akipokea vifaa vya kujikinga na ugonjwa wa corona kutoka katika Taasisi ya Odo Ummy Foundation iliyotoa vifaa hivyo kwa lengo la kuunga mkono juhudi za serikali ili kutokomeza kabisa ugonjwa wa corona .
“kwa nafasi hii ni,iyopewa ya kupokea vifaa hivyo kwaajili ya nyumba za ibada na ikiwa imezingatia pande zote mbili ukristo na uislamu nipende kuwaomba mapadri na mashehe kuendelea kutoa elimu katika maeneo yao ya ibada “Alisema Mkuu wa Wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
Sambamba na hayo Mwilapwa ameendelea kuwakumbusha wananchi kuendelea kuchukua tahadhari hata kama ugonjwa umepungua kwani haujaisha kabisa na kuendelea kujikinga na magonjwa mengine ya milipuko .
Kwaupande wake katibu mtendaji wa Taasisi ya Odo Ummy Foundation Hatibu Kilenga amesema lengo la kutoa vifaa hivyo ni kuendelea kulinda afya za wananchi kwa kuendelea kulinda usafi katika maeneo ya ibada kwa kuwa taasisi hizo zina mwingiliano mkubwa wa watu .
Vifaa vilivyotolewa na Taasisi ya Odo Ummy Faundation ni pamoja na matank pamoja na sabuni ambavyo vitagawanywa katika Taasisi kumi zikiwemo za dini kiislamu na kikristo .
Nae Diwani wa kata ya Chumbageni Saida Gaddafi ameipongeza taasisi hiyo na kuahidi kuvigawa vifaa hivyo katika sehemu zinazotakiwa ili kuendelea kujikinga na magonjwa ya milipuko .
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.