Waziri wa habari Utamaduni sanaa na michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amepongeza tasnia ya habari nchini kwa juhudi za kuhabarisha watanzania juu ya mambo mbalimbali ikiwemo utendaji kazi wa Serikali.
Waziri mwakyembe ameyasema hayo wakati akizungumza na wadau wa vyombo vya habari Mkoa wa Tanga ambapo amesema kuwa watanzania wana imani na tasnia hiyo hivyo ni wakati kwa waandishi wa habari kuzitumia vema kalamu zao na kudumisha amani nchini.
Dkt Mwakyembe amewataka wananchi kujua kuwa fani ya uandishi wa habari ni kazi ambayo inathamani na kuwataka kuacha kuwadharau waandishi wa wahabari sambamba na kuwakumbusha waandishi ambao hawana diploma kwenda kusoma .
“Tumetunga sheria ambayo inawataka wanahabari kuwa na taaluma ya diploma ili tuondokane na dhana ya kuwa kila mtu akifeli sekondari anaambiwa akasome tu uandishi wa habari na ndio maana wanahabari tunadharaulika “,.Alisema Mwakyembe
Pia Dkt . Mwakyembe amepiga marufuku kwa wasimamizi wa mabasi ya abiria ikiwa ni pamoja na madereva na makonda kupiga nyimbo ambazo zimezuiwa na serikali zisioneshwe kwenye runinga kwani zinavunja maadili ya Kitanzania .
“Ni marufuku kwa basi lolote la abiria kuonesha picha za ovyo ambazo tumezizuia zisioneshwe kwenye runinga mchana basi ni chombo ambacho kinapakia kila mtu kwaiyo ni lazima tuchukue hatua kali sana hatupo tayari kuharibu watoto wetu “,.Alisema Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe
Lengo la ziara ya Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo kuja katika Mkoa wa Tanga ni kufuatilia usikivu wa redio ya Taifa katika Mikoa mbalimbali na kwa kuanza wameanzia Mkoani Tanga ambapo pia waliweza kutembelea katika kituo cha matangazo cha Tanga Televisheni na kukipongeza kwa utendaji kazi wake .
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Dkt. Harrison Mwakyembe akiwasisitiza wanahabari wasio na Diploma kwenda kusoma .
Wadau mbalimbali wa habari wakimsikiliza Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.