Afisa mwandikishaji wa Tume ya Uchaguzi Tanga Jiji Daudi Mayeji amewataka Waandikishaji wasaidizi kuzingatia wanayofundishwa katika Semina ya Uboreshaji daftari la kudumu la Mpiga kura awamu ya pili ambalo litaanza tarehe 17-19 mwezi huu wa nne katika Ofisi za Kata.
Mayeji alisema kuwa wamechukua tahadhari zote za ugonjwa wa Corona katika kila kituo cha Mpiga kura na kuwasisitiza Waandikishaji kusimamia kanuni zote kama zinavyotakiwa .
"Nataka niseme kwamba katika semina hii tusiwe wajuaji sana tusikilize na kuzingatia maelezo yote yanayotolewa na wataalamu wa afya kitu cha muhimu ni kusikiliza maelekezo kwa makini na kama mtu hujaelewa na unataka kuelekezwa ni ruksa kuuliza ili upewe ufafanuzi na baada ya hapa tukaweze kutekeleza jukumu kwa ufanisi zaidi "Alisema Afisa uandikishaji wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji
Mayeji aliongeza kwa kusema kuwa katika kila kata kutakuwa na kituo kimoja cha wananchi kwenda kufanya maboresho ya taarifa zao katika daftari la kudumu la mpiga kura tofauti na mara ya kwanza kulipokuwa na vituo vingi .
Sambamba na hayo pia Mayeji aliwataka wale wote ambao hawakupata nafasi ya kujitokeza kurekebisha taarifa zao kwenda katika vituo ili kuboresha na kuweza kupata nafasi ya kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu utakao fanyika october mwaka huu .
Uboreshaji wa taarifa katika daftari la kudumu la mpiga kura pamoja na uandikishaji kwa awamu ya pili unatarajiwa kuanza tarehe 17 ya mwezi wa nne siku ya Ijumaa na kumalizika tarehe 19 ya mwezi wa nne siku ya Jumapili .
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.