Afisa mwandikisha jimbo la tanga Daudi Mayeji amefungua mafunzo ya siku mbili ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura na kuwaapisha waandikishaji wasaidizi wa daftari la wapiga kura mwaka 2020.
Mayeji amesema kuwa dhumuni la mafunzo hayo ni kwa ajili ya kutekeleza wajibu na utaratibu wa uboreshaji daftari la wapiga kura,kupata uelewa wa kutumia mfumo wa bvr kit kwa ufasaha.
Sambamba na hayo Afisa Mwandikishaji jimbo la Tanga Daudi Mayeji amewapongeza waandikishaji hao wasaidizi nakuwasihi watunze vifaa kwani serikali imeridhia zoezi hili kufanyika kwa ufanisi na kuwa na ushirikiano katika zoezi hilo la uboreshaji daftari la wapiga kura.
“Nina hakika baadhi yenu mlishashiriki katika zoezi hili la uboreshaji katika daftari la kudumu la wapiga kura hivyo mnauzoefu katika kuratibu na kusimamia vizuri ninaimani kwa kutumia uzoefu mlionao mtafanya kazi yenu kwa ufanisi mkubwa”,.Alisema Daudi Mayeji Afisa mwandamizi jimbo la Tanga
Kwa upande wao waandikishaji wasaidizi wa daftari la kudumu la wapiga kura Martine Hijja na Clara Materu wameahidi kufanya kazi kwa usahihi pindi watakapofika katika maeneo yao ya uandikishaji .
“Mengi tumefundishwa na tumeambiwa kwaiyo wananchi wanatakiwa kujitokeza ili kuboresha taarifa zao na sisi kazi yetu ni kusaidia watu na tutafanya hivyo “,. Walisema waandikishaji hao ambao ni Clara Materu na Martine Hijja
Uandikishaji katika daftari la kudumu la kupiga kura katika Jiji la Tanga unatarajiwa kuanza tarehe 23 mpaka tarehe 29 ya mwezi wa kwanza ya mwaka huu 2020.
.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.