Viongozi pamoja na watumishi wa Serikali wametakiwa kutoa huduma bora kwa wananchi pamoja na Kutoka katika maofisi na kwenda kuzungumza nao kuhusu kero na changamoto walizonazo ili waweze kuzitatua.
Hayo yamesemwa na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt Hassani Abbas wakati akizungumza na Tanga tv mara alipotembelea kituo hicho ambapo amewasihi viongozi kutekeleza adhima ya Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli inayosisitiza kwenda kuwasikiliza wananchi .
“Tunamiaka minne tangu serikali ya awamu ya tano ya Dkt John Pombe Magufuli aingie madarakani mengi yamefanyika na tumeyaona lakini kubwa niwakumbushe viongozi wa serikali katika ngazi mbalimbali kuhakikisha sisi kama viongozi tunatoa huduma bora kwa wananchi na kuacha kuwa viongozi wa mezani”.,Alisema Dkt Hassani Abbas msemaji mkuu wa Serikali
Pia Dkt Hassani Abbas aliwatoa hofu Wananchi wanaodai fidia Serikalini kwa kupisha miradi mbalimbali ya Maendeleo ambapo amesema ni lazima kila Mwananchi anayedai fidia atapewa kwani dhamira ya Serikali ni kuleta Maendeleo kwa Watanzania .
“Kwenye eneo la fidia nisisistize kwamba sheria zipo na zinapaswa kufuatwa iwe anayetoa eneo ni Serikali kuu au upande wa Jiji au kwenye Halmashauri kwaiyo Serikali ya Rais Magufuli inasisistiza kwa Mwananchi atakayeondolewa kwa kupisha miradi ya Maendeleo lazima atalipwa fidia yake “.,Alisema Msemaji Mkuu wa Serikali
Sambamba na hayo Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt Hassan AbbasI amewataka Watanzania kujenga misingi ya kujitegemea kwa kuwa wazalendo wa kulipa kodi na kufanya kazi kwa bidii kwa Maendeleo ya Taifa letu huku akieleza ni kwa namna gani Serikali ya awamu ya tano ilivyoweza kupambana na rushwa.
“Pale ambapo unapaswa kulipa kodi yako ufanye hivyo naomba kuwakumbusha Watanzania kuwa miaka minne hakuna maajabu mengi sana kila unachokiona kizuri ni sehemu ya kodi yako na ukiona kitu kizuri ukawa hujawahi kulipa kodi ulikwepa ujijue wewe ni msaliti kwaiyo Watanzania lipeni kodi ili tulete Maendeleo ya Nchi yetu “.,Alisema Hassani Abbas
Lengo kuu la kufika kwa Msemaji Mkuu wa Serikali katika kituo cha Matangazo cha Tanga televisheni ni kuwafahamisha Wananchi Maendeleo ya Serikali ya awamu ya tano kwa kipindi cha miaka minne ya Rais Dkt John Pombe Magufuli.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.