Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa amewataka viongozi wapya wa serikali za mitaa waliochaguliwa na kupita bila kupingwa kufanya kazi ya kuwatumikia wananchi wote bila kujali itikadi za vyama kwa maendeleo ya taifa.
Mwilapwa aliyasema hayo wakati wa zoezi la kuapishwa viongozi hao wa serikali za mitaa lililofanyika katika ukumbi wa shule ya ufundi Tanga.
“Tukawatumikie wananchi wote bila kujali itikadi za vyama vyetu sisi tumechaguliwa na kubeba jukumu la kuwatumikia wananchi wetu katika ngazi ya chini ya uongozi kwahiyo twendeni tukafanye kazi “,.Alisema Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
Kwa upande wake mstahiki meya ya Jiji la Tanga Mustafa Seleboss aliwataka Viongozi hao kutatua Migogoro ya Wananchi katika ngazi ya Mitaa pamoja na kutenda haki .
“Lengo na madhumuni ni kufanya kazi kwa ushirikiano kwa sababu wananchi wenu wamewaamini na kuwaona mnafaa kwenda kusaidia Serikali ya awamu ya tano ili kumsaidia Mwananchi mnyonge katika suala zima la Maendeleo “,.Alisema Mstahiki meya ya Jiji la Tanga Mustafa Seleboss
Nae Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji akaeleza taarifa ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kueleza namna Wyama vingine vilivyojitoa katika Uchaguzi huo hali iliyosababisha viongozi wa CCM kupita bila kupingwa .
“Nafasi zilitolewa kwaajili ya kuweka pingamizi kwa Wagombea wa Vyama vyote na pia kamati ya Rufaa ilikaa na kujadili pingamizi ambazo zilikuwa zimewekwa na kutoa maamuzi na katika maamuzi yale jumla ya wagombea 103 wa Vyama vya Upinzani walijitoa na hali hii ndio iliyosababisha Wagombea wa Chama cha Mapinduzi kupita bila kupingwa”,.Alisema Mkurugenzi wa Jiji la Tanga
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Tanga Hamis Mkoba pamoja na Mjumbe wa Chama hicho Suzan Uhinga wamewapongeza Viongozi hao na kuwataka kujenga mahusiano mazuri na wananchi wao .
Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.