Imeandaliwa na Naetwe Kilango;
Katika hali ya serikali kupambana na umaskini kwa wananchi wake, Halmashauri ya jiji la Tanga kupitia idara ya Maendeleo ya jamii, ustawi na vijana imetoa Tsh 37,000,000/= kwa ajili ya kuviwezesha vikundi vya ujasiriamali jijini hapo kuongeza mitaji na kununua vifaa kw aajili ya kukuza miradi yao. Fedha hizo ni mikopo yenye riba nafuu ya 10% toka vyanzo vya mapato vya ndani vya halmashauri, ambapo asilimia tano hutolewa kwa wanawake na tano kwaajili ya vijana.
Akizungumza na waandishi wa habari wa Tanga Television mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii, ustawi na vijana katika jiji hilo Bi; Flora S. Maagi amesema awamu hii wametoa fedha hizo kwa vikundi saba ikiwemo Tuini women group kinayojishughulisha na utengenezaji wa batiki sabuni na kilimo cha mihogo toka kata ya maweni Tsh’s 15,000,000/=, Kichaung’o women group kinachojishughulisha na ufugaji wa ng’ombe toka kata ya Maweni Tsh’s 5,000,000/=, Helepa women group kinachojishughulisha na utengenezaji wa batiki na sabuni za maji toka Nguvumali Tsh’s 3,000,000/= Mbogo women group kinachojishughulisha na ufugaji wa kuku wa kienyeji toka kata ya Kiomoni 5’000’000/=, Rahagani women group kinachojishughulisha na ufugaji wa kuku toka kata ya Duga Tsh’s 3,000,000/= , Tuwezeshane A women group kinachojishughulisha na utengenezaji wa sabuni, kapeti na urembo toka kata ya Magaoni Tsh’s 3,000,000/= na Tuwezeshane B women group kinachojishughulisha na usindikaji unga wa lishe toka kata ya Magaoni Tsh’s 3,000,000/=
Hata hivyo mkuu huyo wa idara amesema wametoa fedha kwa vikundi vichache tuu kutokana na kuwa vikundi vingi vilikosa sifa wakati wa uhakiki, Bi; Shija ameeleza kuwa tayari wameshawajengea uwezo wanawake na vijana na wameanza kusajili vikundi kwaajili ya kupatiwa mkopo tarajali, sambamba na hayo amewataka wanawake na vijana kutumia fursa hii kujikwamua kiuchumi ikiwa ni pamoja na kuanzisha shughuli halali za pamoja, endelevu na zinazopimika, ameongeza kuwa wiki inayoanza watakua kwenye zoezi la uhakiki wa vikundi vinavyoomba mkopo ili kuweza kukopeshwa mkopo wenye riba nafuu, amesisitiza kusema kwamba fedha zipo za kutosha hivyo wanajamii wajiunge kwenye vikundi vya kiuchumi ili wakopeshwe.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.