Afisa elimu sekondari kutoka katika Halmashauri ya Jiji la Tanga Lusajo Gwakisa amesema katika kuadhimisha siku ya vijana duniani ambayo hufanyika kila ifikapo tarehe 12 mwezi 8 kila mwaka wamefanya maandalizi mazuri ili kuweza kusherehekea siku hiyo kwa amani kwani Serikali ya awamu ya tano inawajali vijana .
Gwakisa alisema hayo katika kongamano lililowakutanisha vijana kutoka katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Tanga ili kuweza kukaa na kujadili mambo mbalimbali .
“Katika Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Magufuli inajitahidi kutoa misaada mbalimbali ili kuweza kuwasaidia vijana na ndio maana tunawambia wakae wajadili na kuona ni namna wataandaa mpango wa kuwasaidia wenyewe“ Alisema Afisa Elimu Sekondari Lusajo Gwakisa
Gwakisa aliongeza kuwa lengo la kukaa kikao ni kuwaambia vijana kwa fikra walizo nazo na mawazo waliyonayo wanaweza kukaa na kujadili ni kitu gani ambacho kitawafanya kutengeneza mpango wa maisha yao .
Sanjari na hayo pia Gwakisa aliwataka vijana kuwa na mshikamano umoja na kuwa na mawazo ambayo yatakuwa na tija katika jamii hasa wao wakiwa ni Taifa la kesho .
Kwa upande wake Mwenyekiti wa vijana Wilaya ya Tanga Omary Ayoub aliwasisitiza vijana kuwa na ushirikishwaji katika mambo mbalimbali ya Kiwilaya ,Mkoa na Taifa kwa ujumla ili kuweza kuona ni namna gani wanaweza kusaidiana.
Nao Vijana walioshiriki katika kikao hicho Liliani pamoja na esta walisema wamefurahi kushiriki katika kikao hicho kwani wamejifunza mambo mengi ambayo walikuwa hawayafahamu ambayo yanaweza kuwasaidia katika manero mbalimbali.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.