Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela amewataka vijana kutambua thamani ya miradi mbalimbali inayoletwa na serikali na kuzitumia kama fursa za kujiinua kiuchumi.
Shigela alisema hayo wakati akizungumza na vijana katika Semina iliyoandaliwa na Taasisi ya kiona youth Cordinate iliyolenga kutoa mafunzo kwa vijana juu ya kuzitambua fursa za kimaendeleo zilizopo katika jamii.
“Serikali ya awamu ya tano inawajali sana vijana na Rais anawaamini sana vijana kwasababu mnanguvu na pia ni wabunifu katika kutekeleza majukumu yenu”. Alisema Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela
Kwaupande wake Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji aliwakumbusha vijana kuwa ndio nguvu kazi ya Taifa na kusema kuwa ni aibu kwa kijana kutoka nyumbani asubuhi mpaka usiku akashinda katika mchezo wa bao badala ya kujishughulisha katika kazi .
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la kiserikali la Kiona Youth Cortinate Fatma Fungo alisema lengo la kutoa mafunzo kwa vijana hao ni kuwapa Elimu kuhusu ujasiriamali ,utunzaji wa fedha,uzazi wa mpango na mapambano dhidi ya madawa ya kulevya .
Nao vijana ambao walishirika katika mafunzo hayo walieleza namna ambavyo yamewasaidia kuanzisha vikundi mbalimbali na kuweza kusaidia kujikwamua kiuchumi ,kutunza afya zao pamoja na kujiepusha ma makundi mabaya.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.