Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mustapha Seleboss amewataka vijana Jiji la Tanga kuwa na utayari katika kuanzisha mambo ya kimaendeleo pamoja na kuwa
Mstahiki meya ameyasema hayo katika warsha iliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la kiona youth coordinates ili kuweza kupitia rasimu ya chapisho la mwongozo kwa wajumbe mbalimbali kuhusu uendeshaji wa Baraza la Taifa la vijana .
Seleoss amesema ni vyema Halmashauri ya Jiji la Tanga iweze kuandaa mpango wa kutoa elimu kwa vijana ili kuweza kuwasaidia vijana hayo kutambua sera zao .
“Tatizo vijana wengi wanapenda wanapenda kufanikiwa lakini kujishughurisha hawataki hiyo ndio changamoto kubwa ya vijana wanapenda pepo lakini ukiwambia kufa leo hataki “Alisema Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga
Kwa upande wake mkurugenzi wa kiona youth Coordinates Fatma Fungo ameeleza ni namna gani wanaweza kuwasaidia kwa kujadiliana masuala ya vijana na kuona ni namna gani wanakuja na mawazo ili kusikia malengo makuu.
Nae mwezeshaji wa warsha hiyo Dr Ali Fungo pamoja na vijana walioshiriki Abubakar Soud na Hadija Msenga wakawataka vijana kujitokeza kwa wingi pindi wanapoitwa ili kujadili masuala yao .
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.