Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamiij Jinsia Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu amezindua Majengo mawili moja likiwa ni jingo la Dharura na Jengo jingine kwaajili ya wagonjwa mahututi katika Hospitali ya Rufaa Bombo Mkoani Tanga.
Mhe.Ummy Mwalimu pia amepata nafasi ya kuwapongeza watendaji wa Wizara ya Afya pamoja na uongozi mzima wa Hospitali ya Rufaa ya Bombo iliyoweka historia ya kuleta mapinduzi ya upatikanaji wa huduma za Dharura na huduma kwa ajili ya wagonjwa mahututi katika hospitali za rufaa za Mikoa.
Mhe.Ummy Mwalimu amewashukuru wadau wa Abort ambao wamewezesha kujenga jengo la dharura pamoja na kununua vifaa na kusema kuwa ukijenga huduma za dharura unaokoa maisha kwa asilimia 40.
Amesisitiza Mhe.Ummy Mwalimu kuwa katika mkoa wa Tanga wanajenga Hospitali za Wilaya Tatu Ikiwemo Tanga jiji,Muheza na Korogwe pia wameboresha na kujenga vituo vya Afya kumi na tisa na jiji la Tanga wamepata vituo vinne.
Hata Hivyo Waziri Ummy Mwalimu amesema kuwa wao kama Wizara ya Afya wataendelea kuhakikisha wanaboresha huduma za Afya katika ngazi zote katika ngazi za msingi na sekondari ngazi ya kati pamoja na Hospitali ya Taifa.
Kwa upande wake Dkt.Leonard Subi ambaye ni Mkurugenzi wa Huduma za Kinga kutoka Wizara Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto amesema kuwa wao kama wizara wanaangalia zaidi Ubora kwasababu wanaamini wanapoboresha huduma za Dharura viwango vya vifo vinapungua kwa asilimia arubaini.
“kwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga tayari wana Daktari bingwa mmoja Ambae amepata mafunzo ndani ya Nchi na uzuri ni kwamba Hospitali yetu ya Rufaa ya Kitaifa Muhimbili ina chuo chetu kikuu kimekuwa kinatoa mafunzo kwa Wanafunzi na hivi sasa tuna Wanafunzi takribani ishirini na tisa ambao wanaendelea na mafunzo haya ya dharura katika chuo chetu “Ameyasema hayo Dr Leonard Subi.
Dkt. Subi ameendelea kusema kuwa Mikoa na Halmashauri waendelee kutenga fedha ili waendelee kupeleka wataalamu na watoa huduma za Afya kwenda kujifunza namna ya kutoa huduma bora za Dharura kwa wananchi.
Katika ufunguzi huo Mhe.Ummy Mwalimu amesema mipango hii ni endelevu kwa Mikoa mingine kwani hata Hospitali mpya za Rufaa za Mikoa ambazo Mhe.Rais alitoa fedha zinaangalia sanas wala la huduma za dharura na huduma zote muhimu zinakuwepo na kwa kufanya hivyo zitajenga uwezo Hospitali za Wilaya na hatimaye vituo vya afya kwani zaidi ya vituo 352 vimekarabatiwa ndani ya miaka miwili katika nchi yetu ya Tanzania.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.